Makundi ya Michuano ya Kombe ya Dunia kwa Watoto wa Mitaani yamepangwa ambapo Tanzania (Street Stars) imepangwa kundi la 2
ambalo linaonekana kuwa kundi gumu sana. Mashindano hayo yatafanyika nchini
Brazil katika Jiji la Rio de Janeiro kuanzia tarehe 28/03/2014 hadi tarehe
7/03/2014.
Kundi la Tanzania lina timu za
1. Tanzania 2. Burundi 3. Argentina
4. Philippines 5. Nicaragua Makundi mengine ni Kundi la kwanza
lina timu za 1. Brazil 2. South Africa 3. Liberia 4. Indonesia 5. Egypt Kundi
la tatu lina timu za 1. Kenya 2. Mauritius 3. USA 4. India 5.
Timu ya
Tanzania iliyokuwa ikinolewa na Sylvestre Marsh kabla ya kuugua, itaondoka
Tanzania tarehe 27th baada ya Kuagwa na Serikali ikiwa na msafara wa viongozi 3
akiwemo Mwalimu wa timu, na Rais wa TSC Sports Academy Bw. Altaf Hirani, na
wachezaji 10 wa umri chini ya miaka 16 pamoja na wachezaji waandamizi 2
walioshiriki mashindano haya mwaka 2010 kule Durban Afrika Kusini.
Ikumbukwe
kuwa Tanzania inashiriki mashindano haya kwa mara ya pili mfululizo baada ya
kushiriki kule afrika kusini na kufanikiwa kufika fainali baada ya kuzifundisha soka timu za, Brazil, Phillipines ,
Nicaragua , na baadae kutoka sare na Uingereza moja moja, kabla ya kufungwa
na India kwenye fainali goli moja bila, Tanzania ikifungwa kwa mkwaju wa penalt
zikiwa bado dakika 5 mpira kumalizika.
Kwa kumbukumbu hii Tanzania inaelekea
Brazil ikiwa na dhamira moja tu kushinda kombe hili na kulileta Nyumbani.
Mutani Yangwe (Mwanzilishi na Mkurugenzi wa TSC Academy) ambaye yupo nchini
Uingereza ataondoka kuelekea Brazil tarehe 26 kwa ajili ya kuipokea timu hiyo.
No comments:
Post a Comment