SERIKALI IMETOA TAMKO KUHUSU UHARIBIFU WA VITI ULIOTOKEA KATIKA MCHEZO KATI YA TIMU YA YANGA YA TANZANIA
NA AL-AHLY YA MISRI ULIOFANYIKA KWENYE UWANJA WA TAIFA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE
01 MACHI, 2014.
WAKATI WA MCHEZO HUO,
KULITOKEA VURUGU KUBWA ZILIZOFANYWA NA WATAZAMAJI AMBAPO BAADHI YAO WALING’OA
VITI NA KUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA.
KATIKA VURUGU HIZO, VITI 10 VILING’OLEWA NA KUTUPWA NA ZAIDI YA VITI 40
VILIHARIBIWA.
SERIKALI IMESIKITISHWA SANA NA TUKIO
HILI NA HASA KWA KUZINGATIA JITIHADA KUBWA ZILIZOFANYWA KUHAKIKISHA KUWA NCHI
YETU INAKUWA NA VIWANJA VIZURI NA VYA KISASA NA HIVYO KUTOA FURSA KWA WANANCHI
WAKE KUCHEZA NA KUPATA BURUDANI KATIKA VIWANJA BORA VYA KISASA NA SALAMA.
WIZARA IMEIELEKEZA TFF KUCHUKUA HATUA
KALI KWA WOTE WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA VURUGU HIZO NA KWA KUZINGATIA TARATIBU
ZOTE.
TFF IMEPEWA MAELEKEZO HAYO KUTOKANA NA
UKWELI WAO NDIO WASIMAMIZI WA MCHEZO HUO NA NDIO WALIOOMBA KUTUMIA UWANJA.
KIMSINGI, ENDAPO MATUKIO HAYO HAYATAKOMESHWA
SERIKALI ITALAZIMIKA KUCHUKUA HATUA KALI ZAIDI.
IFAHAMIKE KUWA UWANJA NI MALI YA WATANZANIA WOTE NA HIVYO NI WAJIBU WA
KILA MMOJA WETU KUULINDA NA KUUTUNZA KWA MANUFAA YA MAENDELEO YA MICHEZO
NCHINI.
KWA JUMLA, WIZARA HAITAVUMULIA
UHARIBIFU HUO KUENDELEA. TUSINGEPENDA
KUFIKIA HATUA YA KURUHUSU UWANJA KUTUMIKA BILA WATAZAMAJI AU KUZUIA BAADHI YA
MICHEZO KUFANYIKA HAPO KAMA INAVYOTOKEA KATIKA NCHI NYINGINE. NI VEMA TUKAENDELEZA USTAARABU WETU NA KUWA
WAUNGWANA KILA TUNAPOKUWA UWANJANI KUZISHANGILIA TIMU ZETU.
No comments:
Post a Comment