Jambo la kwanza la
kujiuliza kwanini waamuzi wetu wa
Tanzania hawacheshezi fainali za mataifa ya afrika ? au kwanini waamuzi wetu
hawachezeshi mechi kubwa za vilabu vyetu
vya afrika hili ni swari ambalo kwa
mtanzania yoyote Yule anaweza kukupa jibu sahihi kwa anavyofikiri lakini
kikubwa na cha maana zaidi ambacho watu wanatakiwa kufahamu na kuhitaji kuelewa
ni kwanini haya yote yanafanyika katika nchi yetu ambayo kila kukicha timu zina
lalamikia waaamuzi na kusema hawachezeshi vizuri.
Jambo la kwanza na
kuu kuliko yote je waamuzi wetu wanajua wanacho kifanya uwanjani ? lakini la pekee
na kubwa zaidi ni kuwa kwanini waamuzi wetu hawachezeshi mara kwa mra katika
mechi za klabu hasa katika hatua ya Robo fainali ya klabu bingwa afrika au
kombe la shirikisho au mashindano ya Chan hii ina maana kubwa kwetu kuwa
waamuzi bado Uwezo wao upo katika kiwango cha chini lakini ni waamuzi hawa
ambao wanalalamikiwa kila kukicha kupokea Rushwa za Hari ya juu lakini
inawezekana likawa linasababishwa na ubora finyu wa klabu zetu na ligi yetu ya
Tanzania kuwa hatupo katika ubora
unaostahiri .
Kwa kiasi kikubwa
bara la afrika limegawanyika sana katika ubora wa soka na hata waamuzi hutoka
kwa ubora wa kanda ukitazama vizuri Nchi za afrika Magharibi na kaskazini mwa
afrika ndizo nchi zenye ubora zaidi kisoka na ndizo zinatoa timu mara kwa mara
katika fainali za afrika na kombe la Dunia kwa hiyo kutokana na ubora wa soka
ndipo hata uwezo wa waamuzi unaopatikana
na kuongezeka kwa hari ya juu na hii inasababishwa
na mikiki ya ligi na utimamu wa mwili, leo hii Tanzania ina makamishna watatu
mmoja Zanzibar na wawili bara akiwemo mwanamke mmoja.
Sasa kwa hatua
tuliyopo sasa shirikisho la soka la Tanzania lina kazi kubwa ya kuhakikisha ya
kuwa inafanya kazi ya ziada kutazama ni kwa jinsi gani tunaweza kutengeneza
Safu nzuri ya waamuzi katika soka ya Tanzania Tff ilipiga mkwara kuwa timu
yoyote itakayo lalama kuhusu waamuzi basi itachukuliwa hatua za kisheria kauli
hii ni ya Umwamba zaidi na ya utawala wa mabavu kwa sababu kamati inayotazama
waamuzi katika shirikisho la soka la Afrika kila mwaka inachagua kwa kudonoa
donoa waamuzi kutoka Tanzania hii ina maana CAF imeshajua kuwa Tanzania hakuna
waamuzi wanaoweza kutafsiri sheria kiusahihi kwa asilimia Angalau sitini lakini
hili lina shaka ndani yake wachezaji wengi wa watanzania uwezo wa kutafsiri
sheria za soka ni Mdogo sana ndio maana wanashindwa kucheza ulaya.
Lakini tunahaja ya
kulitazama upya jopo la waamuzi la Tanzania ndani ya shirikisho la Soka kwa
sababu kubwa ni kwamba nani anayetoa tathimini ya Waamuzi hawa kwanini kila
mwaka tunachemsha huwa tunaskia makocha tu wanapata kwenda nje kwa ajiri ya mafunzo
lakini waamuzi wetu sidhani kama wanakwenda mafunzo ya uamuzi wa mchezo wa
mpira wa miguu kwa sababu sheria zinabadilika kila uchao kwa kutazama katika
mitandao wakati Uefa wakiboresha Sekta ya waamuzi kwa kuweka Waamuzi watano
kiwanjani .Leo Tanzania bado tupo katika hatua ile ya kuweka waamuzi watatu.
Je kwa mambo kama
haya unadhani makocha,wachezaji,na waamuzi wenyewe ambao nao wanashindwa
kutafsiri unadhani kuna kitu ambacho tunaweza kufanikiwa kupata mwamuzi hii ina maana kuwa tunahitaji
kuwa na upana mkubwa zaidi wa kutanua wigo wa Elimu hasa wa kimataifa kwa
waamuzi wa soka la Tanzania bila hivyo tutakuwa tunalamikia waamuzi kila siku
kwani inawezekana kuwa kuna mambo ya kina ya kuzingatia katika sekta hii ya
utoaji wa haki kiwanjani.
No comments:
Post a Comment