Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama
Mart Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26
mwaka huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.
Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nooij aliwahi kuwa mkufunzi wa Maendeleo wa chama cha soka cha kifalme cha uholanzi na aliwahi kufanya kazi katika klabu ya EVC 1913 huko marekani na Kazakhstan.Aliwahi kuwa kocha wa Timu ya taifa Burkina Faso chini ya miaka U-20 mwaka 2003 Katika michuano ya kimataifa ya dunia. Mwaka 2004 aliwahi kuwa kocha msaidizi wa muda wa klabu ya nchi mwake ya FC Volendam.
Mwaka 2007 alichaguliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Msumbiji na alifanikiwa kuipeleka timu hiyo katika michuano ya kimataifa ya mataifa ya afrika mwaka 2010 baada ya miaka 12 . Msumbiji ilimaliza ya mwisho katika kundi lake ikitoa suluhu moja na na kufungwa katika kundi lake Baada ya kushindwa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mataifa mwaka 2012 katika mataifa ya afrika , Nooij alijiuzulu kama Meneja mwaka mwaka 2011. Na nafasi yake kuchukuliwa na Kocha wa ujerumani Gert Engels.
No comments:
Post a Comment