Mchezaji wa soka Ismail Gunduz wa SK Rum ambaye ni mchezaji wa Ridhaa huko nchini Austria amepata Adhabu kubwa mara baada ya kumtandika mwamuzi wa mchezo huo ambapo amefungiwa Mechi 70-,Vyombo vya habari vya Austrian vimekaliliwa .
Huku timu yake ikiwa nyuma ya mabao matatu kwa mawili 3-2 Dhidi ya SPG Innsbruck West katika Dakika ya 86 ya Mchezo jumamosi iliyopita , Ismail Gunduz ambaye ni mchezaji wa Ridhaa wa Timu ya SK Rum na ilitokea mara baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano .
Kwa mujibu wa taarifa zilizo ripotiwa na magazeti ya Nchini humo Tiroler Tageszeitung, kijana huyo mwenye miaka 26- Gunduz alimpiga kichwa mwamuzi
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kugongwa kichwa hicho.
Kwa mujibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa kosa kama hilo ni kufungiwa michezo 108.
.
Lakini jambo kama hili liliwahi kutokea katika Ligi kuu soka Tanzania Baina ya Azam fc Dhidi ya Yanga lakini kwa kutokuona vizuri Mwamuzi Israel Mkongo alimtoa Nje kimakosa Beki wa kati wa Yanga
, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, japokuwa Canavaro alinukuliwa akisema kuwa hakumpiga
ngumi mwamuzi wa kati, Israel Nkongo, bali alipigwa na beki wa pembeni
wa timu hiyo, Stephano Mwasika.
Yanga ilivaana na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyomalizika kwa timu hiyo ya Jangwani kufungwa mabao 3-1 huku beki huyo akilimwa kadi nyekundu baada ya kutuhumiwa kumpiga ngumi mwamuzi.
Yanga ilivaana na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyomalizika kwa timu hiyo ya Jangwani kufungwa mabao 3-1 huku beki huyo akilimwa kadi nyekundu baada ya kutuhumiwa kumpiga ngumi mwamuzi.
Je la Kujiuliza ukitazama adhabu aliyopewa Gunduz ya Mechi sabini ni sawa na misimu miwili au mitatu kwa Ligi ya Tanzania lakini ukitzama hivi kwa Tanzania unaweza kutoa Adhabu kama Hii kwasababu Mechi sabini ni muda mrefu kwa maisha ya mchezaji lakini mwasika alikaa muda mfupi sana kwani haikuzidi hata mwaka Je nini cha Kujifunza kwa Taifa la Austria sio tu mechi sabini bali na faini juu ipo haja ya kutazama mambo kwa undani zaidi lakini sitarajii kwa Nchi kama ya kwetu kufanya jambo kama hili siku moja .
Kilichofanyika hapa ni sawa na Kumtukana hakimu ukiwa na kesi ya Ubakaji
Hii imekuwa adhabu ya kihistoria katika ulimwengu wa soka duniani.
No comments:
Post a Comment