HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 April 2010

Kashfa katika kriketi India

 
Mwenyekiti wa baraza la kriketi anakabiliana na madai ya rushwa Baraza linaoloyasimamia mashindano yanayoingiza senti nyingi zaidi ulimwenguni, ligi ya Premier ya India, limemchagua mwenyekiti wa muda, kufuatia mkutano wa dharura kuzungumzia juu ya madai ya mwenyekiti Lalit Modi kuhusishwa na rushwa na uwekezaji katika biashara zisizo halali. Bodi hiyo ya kriketi jana usiku ilimsimamisha kazi Bw Modi, dakika chache tu baada ya fainali ya kukamilisha msimu huu mjini Mumbai. Ligi hiyo, ambayo wengi huifikiria kwamba huchangia katika kustawisha na kuimarisha uchumi wa India, huwashirikisha baadhi ya wachezaji bora zaidi duniani, na ambao huzichezea timu zinazomilikiwa na matajiri wakubwa na wacheza filamu mashuhuri nchini India. Mwandishi wa BBC anaelezea kwamba kwa ligi hiyo kuunganisha kriketi na burudani, ni jambo ambalo limeyafanya mashindano hayo kupata umaarufu mkubwa duniani.  

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers