HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 April 2011

UNDER 23 YAWASILI SALAMA

Timu ya Taifa chini ya miaka 23 imewasili salama Uganda jana saa 1.30 usiku kwa ndege ya Air Uganda chini yz kiongozi wa msafara Hafidh Ally Tahir. -U23 chini ya Kocha Jamhuri Kihwelo ''Julio'' imewasili na wachezaji 20; Nahodha Shaaban Kado, Juma Abdul, David Luhende, Babu Ally, Shomari Kapombe, Jabir Aziz, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Kigi Makasi, Gharib Mussa, Mbwana Bakari, Idrisa Abdulrahim, Innocent Wambura, Khamis Mcha, Amour Suleiman, Himid Mao, Mrisho Ngasa na Salum Telela. -Timu imefikia hoteli ya Sojovalo iliyoko Barabara ya Rubaga hapa Kampala. Leo saa 1.30 asubuhi imefanya mazoezi kwenye uwanja wa klabu ya Express Red Eagles ulioko Wankuluku. -Jioni kuanzia saa 10 kamili timu itafanya mazoezi Uwanja wa Mandela (Namboole) kwa kati ya dakika 45 na saa 1 kujiandaa kwa mechi ya kesho. Mechi ya kesho dhidi ya Uganda 23 (The Kobs) inayofundishwa na kocha wa zamani wa Kagera Sugar, George Ssemogerere itachezwa Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10.30 jioni. Baada ya mazoezi ya U23 ndiyo kutakuwa na mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre Match Meeting) utakaofanyika kwenye ofisi za Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA). -Uwanja huo utatumika kwa mara ya kwanza kesho, kwani kwa kipindi cha miezi sita iliyopita haukutumika kutokana na kuwa kwenye ukarabati. Kobs walifanya mazoezi yao ya leo asubuhi kwenye uwanja huo. -Kocha Julio amesema wachezaji wake wote wako katika hali nzuri kwa ajili ya mechi ya kesho. "Tuko vizuri, tumekuja kupambana. Tunajua Uganda ni timu nzuri, lakini tumejipanga kwa ajili ya kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri kwa mechi ya marudiano itakayofanyika nyumbani,"amesema Julio. -Amesema atataja kikosi kitakachoanza kesho asubuhi baada ya wachezaji kupata kifungua kinywa. -Mechi hiyo imekuwa ikizungumza katika baadhi ya viunga vya Kampala kutokana na U23 kuitoa Cameroon kwenye michuano ya mchujo ya Olimpiki. -Kikosi cha Kobs kina baadhi ya wachezaji wanaochezwa soka nje ya Uganda kama Emmanuel Okwi (Tanzania) na Moses Oloya (Vietnam). Wengine ni Benjamin Ochan, Ayoub Kisarita, Godfrey Walusimbi, Owen Kasule, Patrick Edema, Ivan Bukenya, Sadam Mussa, Mike Mutyaba, Isaac Isinde na Diego Kiiza. Best Regards, Boniface Wambura TFF Media Officer 0767310242

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers