18 August 2012

SONG HUYOO BARCELONA! ARSENAL YATHIBITISHA

 Alex Song,Arsenal FC

Klabu ya soka Arsenal na  Barcelona zimekubaliana kufanya biashara ya kumuuza na kumnunua kiungo wa klabu ya arsenal   Alex Song, klabu ya arsenal imethibitisha hilo  ,Barcelona imekua ikimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa arsenal mwenye miaka 24 kwa mujibu wa klabu hiyo ya arsenal imethibitisha kuwa imekubali ofa ya kumuuza kiungo  huyo.
Music To Barca's Ears
Hawa jamaa wanamuziki mzuri wananiita kwa kunichombeza Lazima niende .
Song atakwenda uispania kujadiliana makubaliano binafsi  ya mishahara na kufanyiwa vipimo vya kiafya.

Mchezaji huyo wa arsenal na wakimataifa wa kameruni alionekana kuwa ni moja kati ya viungo bora katika klabu ya arsenal msimu uliopita na inaonekana kuwa amekuwa gumzo kwa uhamisho wake katika mitaa ya london mara baada ya Robin Van Persie kuhamia Manchester united Akitokea arsenal baada ya klabu hizo mbili kukubaliana kuuziana mchezaji huyo. wakati leo ukiwa ni ufunguzi wa msimu wa ligi ya premier ya uingereza klabu ya arsenal imetoka suluhu ya bila bila  na Sunderland  katika uwanja Emirates. 


No comments:

Post a Comment