11 September 2012

Murray anyakua ubingwa Michuano ya wazu ya US

 

Andy Murray, hatimaye amefanikiwa kuondoa mkosi wa Uingereza wa kungoja kwa kipindi cha miaka 76 kunyakua ubingwa wa mashindano makuu ya Tennis ya Grand Slam kwa wanaume alipomshinda Novak Djokovic katika fainali ya mashindano ya Marekani. Muingereza wa mwisho kutwaa taji hilo alikuwa Fred Perry mnamo mwaka 1936.
Murray,mwenye umri wa miaka 25, alishinda kwa seti tatu kwa mbili, 7-6 (12-10) 7-5 2-6 3-6 6-2 katika kipindi cha saa 4 na dakika 54 katika uwanja wa Arthur Ashe mjini New York.
Katika kipindi cha miezi michache iliyopita Murray pia alifanikiwa kufika fainali ya mashindano ya Wimbledon na pia kushinda nishani ya dhahabu katika michuano ya Olympiki mjini London.
"Nilipotanabahi kwamba nimeshinda ,nilipigwa na mshtuko kidogo. Nilipumua kweli lakini nilijawa na hisia nzito", aliongeza Murray.
Licha ya mafanikio yake mengine,hapana shaka kwamba matokeo haya, yatakuwa na athari kubwa zaidi kwa mchezo wake binafasi na mustakhabali wa tennis nchini Uingereza.
 BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment