13 October 2012

Angel Eaton AONGOZA MASHINDANO YA RIDHAA YA GOLF UGANDA

Msichana mwenye miaka Ishirini na mbili  Angel Eaton kutoka  Tanzania  anaongoza katika mashindano ya  Ridhaa ya Golf kwa alama 73 katika mashindano ya Ridhaa ya wanawake yanayofanyika huko Uganda  ambapo mpaka asubhi ya leo alikuwa akiongoza kwa alama  72 katika kiwanja cha  Kitante 

Bingwa Mtetezi  Flavia Namakula alipiga mipira minne kati ya sabini na sita na hivyo kuhitimisha raundi yake ya tatu ambapo ataendelea tena hapo kesho , MTanzania Hawa Wanyeche  alikuwa wapili mara katika mizunguko mitatu ya mwanzo na kupata alama  par 75 

Watanzania ndio waliionekana kumiliki siku ya leo huku Iddy Madina na  Ayne Magombe wakikamilisha nafasi tano za juu huku wakipiga mipira minne nakuapata alama 76 wakati mwenzake akipiga mipira sita na kupata alama 78 kwa upande wa wanawake .

Mashindano hayo yataendelea tena  kesho kwa mchezo kwa wa wachezaji wawili wawili  
mashindano haya ya siku  tatu yanadhaminiwa na Ndege ya Qatar Airways ,Crown Beverages,Fresh Diary,Nile Breweries,Housing Finance,Orange,MTN,Leading Edge,Soothing Spa,Hwang Sung,Jireh Beauty Products,Saint Augustine University na  Alberto Disco.
 Mashindano ya Ridhaa ya golf kwa wanawake 
  Siku ya Kwanza  1
A. Eaton 73 gross
H. Wanyeche 75
F.Namakula 76
I. Madina 76
A.Magombe 78
D.Naik 78
L.Chingono 79

No comments:

Post a Comment