HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

5 October 2012

UJIO WA Richard Nwoba WAANZA KUZAA MATUNDA

Hivi karibuni, promota maarufu wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Misri Richard Nwoba wa kampuni ya “Louaa Boxing Promotions” alizitembelea ofisi za IBF zilizoko jijini Dar-Es-Salaam ili kuona namna ya kupromoti mapambano ya ngumi katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Bwana Nwoba alikutana na Rais wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi “Onesmo Alfred McBride Ngowi” na kufikia makubaliano ya kushirikiana na makampuni matatu ya Tanzania kupromoti mapambano nanne ya ubingwa wa IBF katika mwezi wa Novemba.
Katika makubaliano hayo mabondia kadhaa wa Tanzania, Kenya na Misri watapambana kuwania mataji manne ya IBF Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi.
Aidha makubaliano hayo yalizaa matunda ya kupromoti mpambano wa ngumi katika Ghuba ya Uarabu ambapo bondia Francis Cheka wa Tanzania atachuana na mbabe wa Oman Amin Saad Mabrook Bait-Saleem katika mpambano wao wa mwezi wa Novemba!
Richard Nwoba ni bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa wa uzito wa juu na sasa makao yake makuu yako katika jiji la Cairo, Misri ambako anaendesha biashara ya ulinzi wa makampuni pamoja na kupromoti ngumi za kulipwa akiendesha kampuni ya “Louaa Boxing Promotions”.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers