HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

29 November 2012

Chaurembo Palasa NI MUONGO

Palasa huyo mweusi
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) inapenda kuueleza umma kuwa taarifa zinazotolewa na kikundi kinachoongozwa na Chaurembo Palasa za kuitisha mkutano wa kuhakiki wanachama ni potofu kwani wanachama wa TPBC ni Kamisheni za mikoa na haina wanachama mmoja mmoja katika ngazi ya taifa. Katiba ya TPBC iliyotoka mwaka 2001 imetamka wazi kuwa wanachama wa TPBC ni Kamisheni za Mikoa.

Hakuna mwanachama wa TPBC anayeitwa Chaurembo Palasa. Kadi ya uanachana anayoitembeza kwenye mitandao ni ya zamani kabla ya katiba ya TPBC kubadilika na kufuta uanachama wake.
Yeye mwenyewe alishiriki kama mwanachama wa kutoa maamuzi ya kikao kilichofuta uanachama wake kwani ilionekana kuwa mabondia wanatumika kuleta fujo kama anavyotumika yeye hivi sasa. Bwana Chaurembo Palasa anakaribishwa kuleta maoni yake kuhusu namna ya kuboresha shughuli za TPBC kama alivyojitokeza na kwenda kulipa ada (japokuwa waliingilia jambo lisilowahusu). Yeye na kikundi chake wanaendelea kuchukua marejesho (refund) ya pesa hizo kila mwezi kutoka kwa Mweka Hazina wa TPBC bwana Boniface Wambura.

Chaurembo na kikundi chake kinachoongozwa na kiongozi mmoja wa chama cha ngumi za kulipwa na ambaye ameamua kuleta fujo ili kufifisha juhudi za TPBC za kuleta maendeleo ya ngumi nchini wanataka kuturudisha kwenye migogoro isiyoisha ya miaka ya 80 na 90 ambayo ilitawala tasnia ya ngumi Tanzania.

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) imepanga kuanza kufanya uchaguzi tarehe 31 March 2013 kuchagua viongozi wapya watakaoiongoza Kamisheni hiyo.

Uchaguzi huo utaanzia ngazi za mikoa kwa kuchagua Makamishna wa mikoa pamoja na Kamati za Utendaji. Kilele cha uchaguzi huo kitakuwa ngazi ya taifa ambako viongozi wakuu kuanzia Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mweka Hazina na wajumbe wa Kamati ya Utendaji watachaguliwa. Nafasi ya Urais ni ya heshima ambapo atateuliwa na Kamati ya Utendaji pamoja ya ile ya Katibu Mtendaji ambayo ni ya kuajiriwa!

Rais wa sasa Onesmo Alfred McBride Ngowi hatatetea tena kiti chake baada ya kuiongoza TPBC kwa takribani miaka kumi (10)! 

Ngowi amewataka watanzania walio na uwezo pamoja na nia ya kuiongoza Kamisheni hiyo wajitokeze ili waweze kugombea nafasi za uongozi. Ngumi za Kulipwa zimekuwa ni ajira na ni vyema tukapata viongozi wazuri wa kuiongoza TPBC ili waweze kutoa nafasi za ajira kwa vijana!

Viongozi wa sasa wa TPBC ni:
Onesmo A.M. Ngowi - Rais
Madara Nyerere - Makamu wa Rais
Nemes Kavishe - Katibu Mkuu
Nicholaus Mallya - Naibu Katibu Mkuu
Boniface Wambura - Mweka Hazina/ Mwenyekiti wa Viwango
Imetolewa na Uongozi
Onesmo Ngowi
Rais
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC)
Dar-Es-Salaam

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers