HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

31 December 2012

Monsieur Patrick Liewing Bievenou Simba Lakini utadumu muda Gani Simba

Kocha mpya wa Simba, Mfaransa, Patrick Liewing pichani, aliyeshika nguo nyekundu mkononi, amewasili leo saa saba za mchana kwa ajili ya kuinoa timu ya Simba.

Uongozi wa Simba, kwa kupitia Katibu Mkuu wao, Evodius Mutawala, alikuwa miongoni mwa wadau wa michezo waliompokea Liewing katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Kocha huyo anawasili huku akiikuta timu ya Simba ikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo Julio, kocha ambaye amekuwa na mapenzi makubwa na klabu hiyo kila wakati kwa kitendo chake cha kukubali kuinoa timu hiyo.

Mengi juu ya ujio wa kocha huyo raia wa Ufaransa, yatasikika baada ya kufanya mazungumzo ya mwisho na kuingia makubaliano rasmi ya kuinoa Simba, yenye kipindi kikubwa cha kurudisha imani kwa wapenzi na wanachama wao.

Simba ilimaliza mzunguuko wa kwanza wa ligi ya Tanzania kwa kushika nafasi ya tatu, nyuma ya timu ya Yanga na Azam FC

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers