HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

14 December 2012

SAM NYAMWEA APEWA MBS NA KIBAKI


Shirikisho la soka la  kenya  (FKF) na Baraza kuu  la taifa  na wanachama wa  (NEC) Wamempongeza  Mwenyekiti wa wa shirikisho hilo  Sam Nyamweya Baada ya kupewa heshima ya Tuzo ya Mkuki wa moran   (MBS) na Rais wa Nchi hiyo   Mwai Kibaki Ikulu ya Kenya jijini Nairobi katika maadhimisho  ya 49 ya siku ya  Jamhuri .

Hii imekuwa Mara ya kwanza kwa kiongozi wa soka kupewa heshima hiyo ya  MBS katika historia ya  Kenya.

Wanachama wa Nec wakiongozwa na Makamu mwenyekiti  Robert Asembo, Elly Mukolwe, Tom Alila, Anjeline Mwikali na  Doris Petra walimpongeza Rais kibaki kwa kuunga mkono juhudi za Nyamwea kwa kazi ya kuleta maendeleo katika soka na kazi kubwa aliyofanya katika shirikisho hilo .

Zawadi hiyo  ambayo hutolewa na Rais  ni kielelezo tosha cha kutambua maendeleo makubwa ya yaliyofanywa na mchezo
unaopendwa zaidi nchini kenya  kwa mwaka jana  

katika mwaka wa kwanza wa uongozi wake tumeweza kuona ligi ya kenya ikipata maendeleo makubwa ligi daraja la kwanza ligi za mikoa manispaa wilaya na ligi ya wanawake 
.
Washirika wakubwa katika udhamaini  Tusker, Coca Cola na kampuni kubwa ya kuzalisha umeme kwa kuonyesha jitihada kubwa katika  kuukuza mchezo huo  .

yapo mambo mengi  sana ambayo yametengamaa ikiwemo waamuzi bora na ubora wa vilabu umeimalika alisema makamu wa Rais
Robert Asembo. 

.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers