HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 December 2012

TFF, ZFA zateta kufungiwa kina Cannavaro


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liko katika mazungumzo na Chama za Soka cha Zanzibar (ZFA) kuhusu kufungiwa kwa wachezaji wote waliokuwa wakiunda kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwenye michuano ya Chalenji iliyomalizika Jumamosi Kampala, Uganda wakiwamo sita waliomo katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Juzi, ZFA ilitangaza kuwafungia wachezaji wote 16 waliokuwa na timu hiyo kutokana na kilichodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu, wakiwamo Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na wenzake watano waliojumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Zambia ‘Chipolopolo’.

Uongozi huo ulidai kuwa wachezaji hao waligawana dola za Marekani 10,000 (Sh. milioni 15) walizopata baada ya Zanzibar Heroes kuibuka mshindi wa tatu katika michuano hiyo kwa kuwafunga ‘ndugu’ zao Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa penati 6-5 kufuatia sare ya 1-1 katika dakika 90 za kawaida.

 Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, amesema kuwa walipokea barua ya ZFA kuhusu kusimamishwa kwa wachezaji hao.

Amesema uongozi wa ZFA utakutana na wachezaji hao Ijumaa kuzungumzia suala hilo.

jana asubuhi tumepokea barua ya ZFA kuhusu kusimamishwa kwa wachezaji hao na wamesema watakutana na wachezaji kwa mazungumzo Ijumaa,” amesema Osiah.

“Sisi (TFF) hatuwezi kuunga mkono vitendo vya utovu wa nidhamu,” .

Hata hivyo, aliongeza kuwa bado wanaendelea kuwasiliana na ZFA kuhusu Cannavaro na wenzake watano wanaopaswa kuwa kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Zambia amabo ni mabingwa wa Afrika.

Wengine waliofungiwa na Cannavaro anayetoka klabu ya Yanga ni kipa Mwadini Ally (Azam), beki Nassor Masoud ‘Chollo’ (Simba), mabeki Samir Haji Nuhu na Aggrey Moris (Azam) na kiungo wa Azam, Khamis Mcha Khamis.

Makamu wa Rais wa ZFA, Alhaji Haji Ameir, alisema kuwa wameamua kuivunja Zanzibar Heroes na kwamba wachezaji hao hawaruhusiwi kucheza katika timu yoyote duniani.

Hata hivyo, ianfahamika wazi kwamba ZFA haina mamlaka ya kufungia wachezaji kucheza kokote kule duniani kwani yenyewe si mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers