HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

29 January 2013

BALOTELI di andare a




 


Manchester City imeanzisha mazungumzo na vilabu vya AC Milan na Juventus kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wake Mario Balotelli, na ripoti zinasema kuwa, Balotelli atauzwa ikiwa vilabu hivyo vitaweza kulipa fedha wanazo taka.
Klabu hiyo imesema mchezji huyo mwenye umri wa miaka 22, anakisiwa kugharibu pauni milioni ishirini na moja mbali na fedha zingine za ziada.
Balotelli hana haraka ya kuuzwa na Manchester City imesema haina mipango ya kupunguza mshahara wake ili aondoke.
Kinyume na matarajio ya wengi Balotelli amesafiri na wachezaji wa Manchester City watakaocheza na QPR katika mechi ya ligi kuu ya premir leo usiku.
Milan ilianzisha mazungumzo na Man City, kuhusu mchezaji huyo kutoka Italia na kuna ripoti kuwa klabu ya Juventus vile vile imewasilisha ombi la kutka kumsajili Balotelli, ambaye alijiunga na Manchester City Agosti mwaka wa 2010 kwa kitita cha pauni milioni 24.
 

Mapema siku ya Jumatatu, naibu kocha mkuu wa Man City, David Platt, alisema kuwa Balotelli hatajiunga na AC Millan mwezi huu.
Siku ya Ijumaa wiki iliyopita, kocha wa Man City Roberto Mancini, alikariri hana nia ya kumuuza kuwa mchezaji huyo kutoka Italia.
Balotelli ambaye amefunga goli moja baada ya kucheza mechi kumi na nne msimu huu, amekumba na kashfa nyingi tangu aliposajiliwa.
Tukio la hivi karibuni, likiwa mzozo kati yake na Mancini katika uwanja wao wa mazoezi mwanzo wa mwezi huu.
Makamu wa rais wa AC Milan Adriano Galliani amesema ikiwa Manchester City itapunguza bei ya mchezaji huyo, basi huenda wakamsajili.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers