HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 January 2013

HOWARD WEBB KATIKATI MAN U VS LIVER !!! TEH TEH TEH

Mwamuzi Howard Webb ameteuliwa kuchezesha mechi ya ligi ya premier kati ya  Manchester United's dhidi   Liverpool
.
Hii itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011 alipochezesha  kombe la FA na mechi kubwa zaidi baada ya kuchezesha kombe la Dunia 2010.

Katika mechi hiyo  Manchester United ilipewa  penalty baada ya   Dimitar Berbatov kuangushwa na  Daniel Agger.
Nahodha wa  Liverpool Steven Gerrard alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya  Michael Carrick katika mechi hiyo iliyokuwa na burudani kwa kipindi kimoja, united ilishinda bao moja sifuri .

 Saa kadhaa baada ya mchezo kumalizika  ,Mshambuliaji wa  Liverpool  Ryan Babel alituma ujumbe kwenye mtandao wa twita :Akisema  "Na wanamwita moja kati ya  mwamuzi bora ? Huu ni utani . SMH [shaking my head--- Natikisa kichwa ]."

Pia alitengeneza picha ya mwamuzi huyo  akiwa amevaa jezi ya united mtandaoni .


  FA ilimpiga faini  Babel £10,000 na kuwa mchezaji wa kwanza kutuhumiwa kutoa jumbe mbaya katika mtandao wa twita  .


 Liverpool na  United wamekutana mara tano baada ya mechi hiyo  ,huku   Phil Dowd na  Mark Halsey wakichezesha mechi mbili wakati  Andre Marriner akichezesha iliyosaria  .


 Kuna tetesi za chinichini kuwa  Webb ni mshabiki wa  Manchester United ,hii inamaana kuwa kuteuliwa kwake kuchezesha mechi ya jumapili italeta hofu na kutoamini kila kitakachofanywa na mwamuzi huyo  .

Aidha mwaka jana mashabiki wa  Man city walilalama pale mwamuzi huyo alipochezesha mechi kati ya city dhidi ya Newcastle wakati timu hizo za city na united zilipokuwa zikufukuzana katika kuwania ubingwa.
mashabiki wa city waliamini kuwa webb angeibeba united kwa kusaidia Newcastle ishinde .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers