HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 January 2013

Seattle Sounders YATUMA WAWAKIRISHI WA KUNDESHA SEMINA TZ



Wawakilishi wawili wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani wataendesha semina kwa wadau wa michezo hapa nchini katika ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.

Wawakilishi hao ni beki wa timu hiyo, Marc Burch na kipa aliyestaafu ambaye kwa sasa ni mtangazaji , Kasey Keller .

Wakiwa nchini, wachezaji hao wataendesha semina kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na shule za msingi katika siku na muda ambao utangazwa hapo baadaye. Z

iara hiyo ni moja ya kukuza ushirikiano baina ya Seattle Sounders na wadau wa michezo nchini na ikumbukwe kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua mchezaji nyota wa Tanzania, Mrisho Ngassa kucheza mechi ya kihistoria dhidi ya timu ya Manchester United.
Kwa kushirikiana na Washington Global Health Alliance (WGHA), wawakilsihi wa timu hiyo pia watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani Arusha ikiwa pamoja na World Vision, taasisu ya PATH na Chuo kijulikanacho kwa jina la Washington State University’s Paul G. Allen School for Global Animal.

”Ziara hii itadumisha na kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania, “ alisema Mmiliki wa timu hiyo, Joe Roth ambaye pia alisema Kesey na March watakuwa mabalozi wakubwa wa timu yao katika ziara hiyo.

Alisema kuwa wajumbe hao pia watatembelea vivutio vya utalii kama Ngorongoro Crater na jiji kubwa la Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Marekani iliingia katika ushirikiano na WGHA mwaka 2009. Mpango huo una lengo la kushughulika na masuala ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers