28 January 2013

kutokana na makosa ya uchapaji

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0gnG_Ug3J33LMGzse8GN8uZNnGphFMklVAoAhyLEn9F6TWMFWKV14F6bXOYc0Undm6QTisqfTvdq2TmxSDxT4VBx0c3kznGCY3Y37ip6gKDSbTFkQ3XMsus4PU3DbCwJq49Csbs1AAdc/s400/osia+angetilr.jpg


 
 
1.   Kamati ya Uchaguzi ya TFF inawaarifu wadau wa soka kuwa kutokana na makosa ya uchapaji, pingamizi iliyowekwa na Nd. Paul Mhangwa dhidi ya maombi ya kugombea uongozi TFF ya Nd. Mugisha Galibona na Nd. Vedastus F.K. Lufano, wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 2 (Mara na Mwanza) haikuchapishwa kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa awali leo (Januari 27, 2013). Mnaarifikuwa kuwa Nd. Mugisha Galibona na Nd. Vedastus F.K. Lufano wamewekewa pingamizi na Nd. Paul Mhangwa ambalo lilipokelewa Januari 22, 2013.
 
2.   Kamati ya Uchaguzi ya TFF itakutana Jumatano tarehe 30/01/2013 saa 4 kamili asubuhi kujadili pingamizi hizo. Waombaji uongozi waliowekewa pingamizi na wawekaji pingamizi wanaarifiwa kufika kwenye kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF tarehe 30/01/2013 saa 4 asubuhi wanajulishwa kuwa barua za mwito wa kuhudhuria kikao hicho zimetumwa kwao kupitia anuani za barua-pepe zilizoonyesha kwenye fomu za maombi ya uongozi na taarifa za pingamizi.
 
Angetile Osiah
Katibu
Kamati ya Uchaguzi TFF

No comments:

Post a Comment