28 January 2013

Brazil yafuta uzinduzi wa siku 500 kueleekea Kombe la Dunia


 http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/81/Dilma_Rousseff_-_foto_oficial_2011-01-09.jpg/175px-Dilma_Rousseff_-_foto_oficial_2011-01-09.jpg

Raia wa Brazil wanaomboleza vifo vya wenzao 233 waliokufa kwenye klabu ya usiku katika mji mdogo wa Santa Maria, usiku wa kuamkia jana. Zaidi ya watu 100 walijeruhiwa kwenye mkasa huo wa kutisha, huku miongoni mwa waliookoka wakielezea namna wenzao walivyonasa kwenye jengo la klabu hiyo ya Kiss lililokuwa na mlango mmoja tu wa kutokea na kufa kwa kupaliwa na moshi na mkanyagano. Wengi wa waliokufa na majeruhi wanahofiwa kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Waziri wa Afya, Alexandra Padilha, amewaambia waandishi wa habari kwamba kwa sasa serikali yake inajaribu kuokoa maisha ya wale inaoweza. Rais Dlima Rousseff aliyeripotiwa kuguswa vibaya sana na mkasa huo, amekatisha ziara yake nchini Chile na kurudi nyumbani, na serikali yake imefuta uzinduzi wa siku 500 kueleekea Kombe la Dunia linalochezwa mwakani nchini humo, ambao ulikuwa ufanyike leo

No comments:

Post a Comment