HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 January 2013

MAALIM SEIF KUKTA UTEPE MAPINDUZI CUP


 
Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad anatarajiwa kufungua rasmi michuano ya kombe la mapinduzi inayotarajiwa kuanza rasmi hii jioni ya leo ambapo michezo miwili itapigwa katika uwanja wa Aman huko Zanzibar.

Katika mchezo wa kwanza Bandari watakuwa wakikutana na Tusker ya Kenya na mchezo wa usiku ambao hasa ndio wa uzinduzi utakuwa ni kati ya Simba na Jamhuri ya Pemba.
Maalimu Seif amealikwa na waandaaji wa michuano hiyo ambayo bingwa wake mtetezi ni Azam FC ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuelekea kusheherekea miaka 49  ya mapinduzi ya Zanzibar michuano ambayo pia hufanyika kila mwaka .
Akiongea na Rockersports msemaji wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo Farouk Karim amesema,
Tayari timu za Tusker, Jamhuri  ya Pemba na Simba zimekwisha kuwasili Zanzibar tangu jana na taarifa zinasema Azam , Coast Union na Mtibwa zinatarajiwa kuwasili huko hii leo . Tiketi zilizo arifiwa mapema kuwa zinatengenezwa nje ya nchi zimeshawasili na zimetoka nje ya nchi.
Forouk ametaja viingilio kuwa ni kwa mchezo wa kwanza jukwaa la Urusi 1000,mzunguko 2000, VIP 5000. Usiku 2000, 3000, VIP 10000.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers