28 February 2013

BOBAN NA MIKASA SOKA SIMBA SPORT CLUB


 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwrdXIT-wR0cGeP-DulUw-E0vcStkKJY_W6wsbpydb8ZNYgYxqINNRC0hfg1Iw5qLxr2-oGjRxJqJZ6k816Pk9itJCGH2zTnb7RYsKmyRQ-Wj8wWU9GRJr_F9tuDbctnQCfTooxTAeuEGm/s1600/boban.jpg

Kiungo Haruna Moshi 'Boban' wa Simba hatakuwamo katika kikosi cha timu yake kitakachosafiri kesho kwenda Angola kucheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Recreativo de Libolo kutokana na majeraha,.
 Boban aliondolewa tangu juzi katika kikosi chao kitakachoondoka kesho alfajiri kwenda kujiandaa kwa mechi hiyo watakayojaribu kubadili matokeo na kusonga mbele baada ya kukubali kipigo  cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa wiki iliyopita.

Daktari wa Simba, Cosmas Kapinga, amesema kuwa Boban hajafanya mazoezi na wenzake tangu walipomaliza mechi ya ligi ya Bara dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo walilala bao 1-0. Daktari huyo aliongeza kuwa kutokana na kutokuwa 'fiti', Boban na mshambuliaji wao yosso, Edward Christopher wameondolewa na kocha wao Mfaransa Patrick Liewig katika mipango yake kwa ajili ya maandalizi dhidi ya Libolo
.

No comments:

Post a Comment