6 February 2013

NIGERIA YAUA 4-1 MALI



Nigeria imeifunga mali  magoli 4-1, katika   mchezo wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Afrika.
Elderson Echiejile amefunga magoli mawili katika dakika ya 25 na 30.

Goli la tatu limefungwa na Emenike katika dakika ya 44 baada ya mpira aliopiga kumgonga Momo Sissoko wa Mali.
Kipindi cha kwanza kimemalizika na sasa ni mapumziko, Nigeria ikiongoza kwa magoli 3-0.
Emmanuel Emenike
Ahmed Musa amezidi kufifisha matumaini ya Mali kucheza fainali baada ya kupachika goli la nne dakika ya 60.
Mali haikuonyesha kukata taama japo muda japo muda ulizidi  kuyoyoma, kwani katika dakika ya 70 Cheikh Diarra aliifungia bao timu yake.
Seydou Keita and Sunday Mba
Nigeria kuingia nusu fainali waliwabwaga Ivory Coast, timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kucheza fainali kutokana na ubora wa wachezaji wake.
Katika mchezo na Ivory Coast, Nigeria walishinda magali 2-1.
Nayo Mali iliwatoa wenyeji wa mashindano Afrika Kusini kwa njia ya mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu hizo kucheza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1-1.
 Nigeria fans
Timu nyingine katika nusu fainali za Afcon ni Ghana itakayokwaruzana na Burkina Faso. Ghana waliitoa Cape Verde katika hatua ya robo fainali kwa magoli 2-0, huku Burkina Faso wakiifunga Togo kwa goli 1-0.

No comments:

Post a Comment