6 February 2013

UMBALI WA SAFARI WAMNYIMA ETO'OO NA WENZAKE KUTUA BONGO

 

Imeripotiwa kwamba nahodha wa timu ya Taifa ya Cameroon Samuel Etoo amejiondoa kwenye kikosi chake kitakachocheza na Taifa Stars kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki february 6 2013 uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Mwanzoni Kocha wa Cameroon aliomba radhi kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuchelewa kufika Tanzania na akatoa ahadi kwamba mpaka february 6 asubuhi ana imani wachezaji wote watakua wamewasili.

Sababu hasa ambazo zimemfanya Etoo kushindwa kuja Tanzania safari hii ni matatizo ya mgongo unaomsumbua kwa sasa.
 kocha wa Cameroon amesema sababu zilizofanya wachezaji wengine kuchelewa kufika Tanzania ni nchi za mbali wanapofanyia kazi, wanacheza Ulaya hivyo ni safari ambayo sio fupi.

No comments:

Post a Comment