HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 March 2013

SIMBA YATOKA I C U YAHAMIA THIETA

Mshambuliaji wa Simba Haruna Chanongo akipiga pasi huku beki wa Coastal Union Mbwana Hamis wa Coastal Union wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union(pallanjo picture)
Timu ya soka ya Simba leo  imeanza kupata fahamu baada ya  kuichapa Coastal Union mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufufua matumaini ya kulejea katika hari ya kawaida   kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa leo.

Baada ya kushinda mechi ya leo ,  Simba SC inafikisha  alama  34, baada ya kucheza mechi 19, na kubaki nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye alama  37, wakati Yanga inaongoza kwa alama   45. 

Hadi nusu ya kwanza inamalizaka  Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Coastal walianza kipindi nusu ya pili ya mchezo , wakipeleka mashambulizi  mfululizo langoni mwa Simba  lakini Abel Dhaira aliweza kupangua mashuti ya washambuliaji wa Coastal


Mrisho Khalfan Ngassa alifungua karamu ya ushindi kwa  Simba dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza, baada ya kumchambua kipa Shaaban Kado, akimalizia pasi safi ya Rashid Ismail.
 
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Mrisho Ngassa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union uliochezwa uwanja wa Taifa (pallanjo picture)
 Haruna Chanongo alipigilia msumari wa pili kwenye ‘goli ’ la Coastal kwenye dakika ya tatu wa muda nyongeza akimalizia kazi nzuri ya Ngassa, kufuatia shambulizi la kushitukiza.

Kipindi cha pili, Coastal walianza kwa kasi na kufanikiwa na kupata bao la kufutia machozi dakika ya 50, lililofungwa na kiungo Razack Khalfan aliyeunganisha krosi ya Twaha Shekuwe.

Simba SC ilichelewa kuingia uwanjani na kukosa hata muda wa kupasha misuli, kutokana na matatizo ya kufungiwa hotelini. 
 
Kikosi cha Simba SC; Abel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Hassan Hatibu, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Rashid Ismail, Abdallah Seseme, Haruna Chanongo na Mrisho Ngassa.

Coastal Union; Shaaban Kado, Hamad Hamisi, Abdi Banda, Mbwana Hamisi, Philip Mugenzi, Razack Khalfan, Daniel Lyanga, Mohamed Athumani, Deangelis da Silva, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Joseph Mahundi

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers