HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

18 April 2013

NENDA KWA AMANI BIBI


 Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana h
Viongozi wa Tanzania na Zanzibar walikuwa miongoni mwa waombolezaji waliohudhuria mazishi ya mwanamuziki mkongwe wa Kisiwani Zanzibar Fatma binti Baraka, aliyesifika kama Bi Kidude.
Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema kuwa watu wengi, walikuwa na majonzi kwani wengi walimuona kama bibi au nyanyao
Wengi walitaka kujionea ili kuthibitisha habari za kifo chake.
Inaaminika alikuwa na zaidi ya miamoja na alikuwa mtumbuizaji wa nyimbo za Taarabu
Aliendelea kutumbuiza wengi licha ya umri wake.
Mnamo mwaka 2005, alituzwa kwa mchango wake katika fani ya muziki wakati wa mkusanyiko mkubwa wa wanamuziki duniani
Mamia ya wanawake waliomboleza nyumbani kwake kabla ya mwili wake kupelekwa kwa maombi kisha mazishi.
Alizikiwa kijijini kwao Kitumba, ambako rais Jakaya Kikwete alitoa heshima zake za mwisho.
Duru zinasema Bi Kidude alitumbuiza wengi na watu walimpenda kwa miondoko yake.
Inaarifiwa Bi Kidude alianza kuimba taarabu mwaka wa 1920
Siku rasmi ya kuzaliwa kwa Bi Kidude haijulikani lakini kuna tetesi liwa alizaliwa mwaka 1910.
uu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib (kulia)'Diamond Plutnum', akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao  Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.
 
Mamia ya watu wakiwa nyumbani kwa kidude tayari kuelekea msibani

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers