HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

23 May 2013

CAMERUNI YAPATA KOCHA MPYA ANATOKEA DEUTSCHELAND

 
 Shirikisho la soka la Cameruni  limemteua  Volker Finke kuwa kocha mkuu wa timu hiyo Televisheni ya taifa ya nchi hiyo imetangaza majira ya saa mbili usiku  katika kipindi cha   newscast.

Mzee huyo mwenye miaka 65-raia wa ujerumani    atakiongoza kikosi hicho hadi mwaka ujao huku akitarajiwa kuongoza timu hiyo kwa miaka minne zaidi . ofa ya kutafuta kocha wa cameruni ilitangzwa mwezi  April 22 ambapo maafisa wa shirikisho la soka cameruni walitoa majina ya watu walio omba kazi hiyo  huku makocha nguli kama Domenech, Eriksson, Lechantre na Finke ambaye ndiye aliyepata kazi akiwemo na anachukua nafasi ya Jean Paul Akono raia wa cameruni ambaye aliamua kutokuomba kazi hiyo ,
kocha huyo anavibarua vigumu katika timu hiyo ikiwemo  kuifunga timu za  Ukraine, Togo na Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa kongo . lakini watu wengi wanaamini kuwa mkufunzi huyo ataanza kazi hiyo mapema zaidi kutokana na hari ya kiafya ya kocha huyo wa sasa japokuwa shirikisho halijatangaza hasa ni lini mkufunzi ataanza kazi rasmi ya kuionoa timu hiyo .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers