HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

30 May 2013

JULIO CESAR AKUBALI KUFANYA MAZUNGUMZO NA ARSENAL

Julio Cesar QPR Brazil

Mlinda mlango Veteran na mdakaji mahiri wa mashuti ya mbali wa brazil anafanya mazungumzo na klabu moja hapa London.
Mlinda mlango huyo wa Queens Park Rangers Julio Cesar amesema anafanya mazungumzo na klabu moja ambayo hakutaka kuitaja jina kwa mujibu wa  Daily Mirror.
Mchezaji huyo mwenye miaka 33-alijiunga na   QPR wakati wa kiangazi akitokea  Inter Milan, lakini anaonekana kukihama klabu hicho baada ya kushuka daraja.
MBrazili huyo ambaye ni hodari kwa kuzuia mashuti alihusishwa  mara kdhaa kutakiwa na klabu kubwa za jiji la London na anatarajiwa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani .

Cesar ameshakubali kuwa yupo katika mazungumzo na  moja ya vilabu vikubwa katika jiji la London ,na inaaminiwa kuwa  Arsenal ndio wahusika wakuu katika kutaka huduma za mchezaji huyo , na wamekuwa sokoni kutafuta mlinda mlango mpya baada ya kutoridhishwa na mlinda mlango wa sasa  Wojciech Szczesny.
Aidha wamekuwa wakimhitaji pia  Asmir Begovic kutoka  Stoke na mlinda mlango wa  Sunderland’s Simon Mignolet wamekuwa wakihusishwa kuhamia  Gunners, lakini  Cesar anaoneka kuwa bei rahisi kuliko wengine kwani anagharimu pauni  £5million.
Katika maisha yake ya Badae, Cesar anasema : “Ninafanya makubaliano na klabu nyingine hapa Uingereza na za Nchi nyingine lakini bado hakujawa sawasawa
“Niafuatilia zaidi Brazil na nina mkataba  QPR, lakini nitatakiwa kuonyesha kuwa bado ninauwezo wa kuitwa kwenye kikosi cha  2014.”
Arsenal pia imehusishwa na  Mchezaji mwenza wa Cesar’s QPR Loic Remy, ambaye amekuwa kivutio cha wengi  Loftus tangu aliposajiriwa  Marseille mwezi  January.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers