HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 May 2013

KWAHERI EVERTON "Everton itakuwa karibu na mimi katika maisha yangu yote ."KARIBU OT


The message posted on Man Utd's Facebook page on Thursday afternoon 

David Moyes Ametia saini kandarasi ya miaka sita kuifundisha klabu ya Manchester United na ataanza kazi ya kuifundisha timu hiyo julai mosi mwaka huu .
Moyes,  Ambaye  anamaliza miaka 11 akiwa kocha wa Everton timu yenye maskani yake  Goodison Park, ndiye mtu aliyepewa chapuo na mkufunzi wa timu ya Manchester united Sir Ferguson's kule  Old Trafford.
Moyes, 50, alikuwa hana kandarasi yoyote na timu yake ya zamani . 
 
"Tumekubaliana na  David Moyes," Amesema  Ferguson,ambaye alitangaza kustaafu Jumatano  Baada ya kuhudumu miaka 26 akiwa na .
 "David ni mtu anayeweza kufanya kazi hii na ana misimamo ya hali ya juu na nilishawahi kuzungumza naye mwaka 1998 kuhusu kuwa kocha msaidizi katika klabu ya Manchester united
"Hakuna maswali  ana vigezo vyote tuna mnatazamia kuwa kocha wetu ."
Moyes, ambaye atatambulishwa kama kocha wa Machester uited  "Hivi karibuni", "hii ni heshima kubwa sana kwangu"  Kuchaguliwa kuwa kocha mpya wa Manchester united na hasa ukizingatia kuwa ni mabingwa wa ligi ya uingereza .
"Ni jambo zuri sana kwangu na kwa Sir Alex mweneye kuona kwamba naweza kuvaa viatu vyake aliongeza raia huyo kutoka uskochi ," . 
"Najua kazi hii ni ngumu kiasi gani ! kwani kufuata nyayo za kocha kama Ferguson , Lakini nafasi ya kuingoza klabu kama Manchester  united sio kitu ambacho kinakuja kirahisi na ninatazama zaidi kuangalia msimu unaokuja nini kitafanyika ."
Moyes, ameelezea kuwa ana kila jambo la kufanya kuitengeneza manchester na kuendeleza yale ambayo yameshafanywa na klabu hiyo aidha  chief Ed Woodward, ametoa heshima zake kwa kocha huyo wa zamani wa  Everton kwa sasa atakuwa anatimiza majukumu yake ya mwisho katika Everton 

"Nilikuwa na kazi nzuri sana na wakati mzuri pale Everton, na tukiongozwa na watu shupavu  na bodi ya wakurugenzi , Na wachezaji wakubwa ,kutoka sasa hadi mwishoni mwa msimu, nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha tunamaliza tukiwa katika nafasi nzuri kwenye ligi .
"Mashabiki wa Everton' ni wazuri sana wameifanya miaka yangu kumi na moja kuwa bora zaidi  hapa  Goodison nina farijika vya kutosha na ninwashukuru kwa ushirikiano wao waliounyesha kwangu na kwa wachezaji .
 
 Everton itakuwa karibu na mimi katika maisha yangu yote ."

Everton ilitoa taarifa kupitia mwenyekiti wa timu hiyo ,Kwa niaba ya klabu , ninachukua nafasi hii kumshukuru David kwa msaada mkubwa alioutoa tangu alipoichukua klabu hiyo Mwezi  March 2002. amekuwa kocha Bora ."
Moyes amaeonekana kuwa ndiye mtu sahihi wa kuifundisha Man united akitokea Everton kwenda kusawazisha huzuni zilitokea mwishoni mwa juma hili baada ya kutokea uvumi wa kujiuzulu kwa Ferguson .
Ferguson,ambaye atabakia Manchester kama mkurugenzi na Balozi ,alikuwa na mahusiano mazuri na mrithi wake wakati wake alipokuwa kocha wa timu hiyo Tangu alipokuwa kocha wa Preston North End.

Moyes alikwisha sisitiza hatofanya maamuzi kuhusu mustakbari na Everton mpaka mwisho msimu huu na sasa amekubali kufanya kazi ambayo waliowengi wanaamini anao uwezo wa kuifanya amekuwa kocha bora zaidi hasa katika matumizi ya alipokuwa Everton na ameweza kuhimili ligi ya uingereza na aliwahi kuifikisha katika hatua za mtoano za kufuzu ligi ya mabingwa ulaya licha kufungwa na Vilareal ambao msimu uliopita walifika nusu fainali . 
  New Manchester United boss David Moyes
Moyes hajawahi kushinda kombe lolote akiwa  Goodison Park lakini anaweza kufanya hilo akiwa na  United's  - na hakuna shaka   Ferguson - atakuwa amevutiwa na uwezo wa David kuifanya iwe hai japokuwa amekuwa na Bajeti finyu .
Kwa sasa ana kazi moja kubwa ya kutetea taji alilolitwaa Ferguson's  na atakuwa na bajeti ya usajiri tofauti na alivyokuwa Everton  . 
Moja kati ya kazi kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa anabamkisha Wayne Rooney,  mchezaji huyo alishasema kuwa anataka kuondoka majuma mawili yaliyopita lakini anaweza kuendelea kusalia united kama atapata uhakika wa kutumika na  Moyes's  na kuwemo kwenye mipaango yake .
Moyes anatakiwa kushinda taji la mabingwa ulaya taji ambalo walishinda mwaka 2008 dhidi ya Chelsea kule  Moscow  .
Wakati huohuo ,kocha wa  Wigan  Roberto Martinez na wa  Swansea  Michael Laudrup wamehusishwa  na kujiunga na klabu ya  Goodison Park kuziba nafasi ya  Moyes. 
  

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers