HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 May 2013

MABONDIA WAANZA UTORO MAZOEZI NGUMI ZA RIDHAAMazoezi ya timu ya taifa ya ngumi za ridhaa yameendelea kudoda kutokana na mabondia wachache kujitokeza yanakofanyika kwenye uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo inajiandaa kushiriki mashindano ya ngumi ya kuwania ubingwa wa Afrika yaliyopangwa kuanza Juni 20 hadi 30 nchini Mauritius.

 katibu mkuu wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT), Makore Mashaga amesema tangu mazoezi hayo yaanze ni mabondia wanne tu walioripoti kambini.
Mashaga aliwataja mabondia waliripoti kuwa ni Idd Pialali, Ibrahim Tamba, Victor Njaiti na Hamad Furahisha.
Aliwataja mabondia ambao bado hawajaripoti kuwa ni Selemani Kidunda, Abdul Rashid, Gurashid Rashid, Haruna Swanga, Seif Hoza, Christian John, Hamdan Issa, Elias Damson, Twalib Athuman, Ismail Italiano, Hashim Simon na Abdul Rashid.
Naye kocha mkuu wa timu hiyo, Remmy Ngabo, amesema ni vigumu kuwa na progamu nzuri ya mazoezi kama mabondia waliwasili ni wachache kiasi hicho

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers