HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

30 May 2013

LEORNAD TADEO UNATANIA AU UKO SERIOUS KWA SWARI HILI

Mkurugenzi wa michezo Leonard Tadeo akishangaa jambo na Beatrice singano wa Airtel



Mpenzi msomaji wa kurasa hii wiki hii kampuni maarufu ya simu za mkononi  ya Airtel ilizundua Program ya ukuzaji wa soka kwa vijana ijulikanayo kama Airtel  rising star huku mkurugenzi wa michezo Leornard Tadeo akitoa nasaha kuwa kampuni hiyo ya simu kuwa  imekuwa ikifanya maandalizi ya soka la vijana kimashindano kwa mwaka wa tatu sasa  kauli ambayo iliungwa mkono na viongozi wa tff kuanzia kaimu katibu mkuu Sunday Kayuni na Makamu wa Rais wa tff Ramadhani Nasibu .

Lakini katika jambo ambalo alikuniingia akilini mkurugenzi wa michezo wa wizara ya habari utamaduni na mchezo Leornad Tadeo aliuliza swari kuwa lazima tujiulize wale vijana wa kwanza ambao walitengenezwa kwa mwaka wa kwanza hadi leo hii wako wapi ?.
Ningekuwa mimi nisinge uliza swari kama hilo lazima kufikilia kidogo kwa sababu ukiwa kama mkurugenzi wa michezo wa wizara ndiye unayetakiwa kujua maendeleo ya programu ambazo mnaziendesha zinaanzia wapi na zinaishia wapi hii ni hatari sana kama mtu aliyepewa dhamana anauliza vijana wako wapi sasa sisi tusiopewa dhamana hiyo tuulize kitu gani ?
kwakweli Sekta ya michezo hasa wizra ya michezo inaeendelea kuwashngaza wananchi kama sio kuwafedhesha kwa swari hili ambalo ameuliza mkurugenzi huyu ni wazi kwamba wizara hii ambayo inaongozwa na Waziri Fenera Mukangara akisaidiwa na Amos Makala haitaweza kutufikisha popote katika sekta ya michezo habari na utamaduni kazi kubwa ya wizara hii imekuwa kujadiri mapato ya uwanja wa taifa hasa wakati wa simba na yanga kwani ndio sehemu ambayo wanajua kuna pesa lakini kwa kutokujua kuna viwanja vingi vya serkali ambavyo viko katika hari mbaya zaidi kwani ukiacha Azam fc timu nyingine karibu zote utumia viwanja vya serikali au mikioa binafsi na kwa bahati mbaya viwanja vingine vimepewa majina ya wakuu wa nchi waliolileta taifa heshima lakini ukienda kuvitazama viwanja hivi havina tofauti na vyoo wa jumuiya tena vya uswahilini!

Mh Tadeo kwakweli umewashangaza watanzania kuuliza kuwa vijana wale wako wapi sisi tulitegemea kuwa umepata jibu la vijana hawa wako wapi kinachoonekana hapa wizara hii inasimamia sera kimaandishi na sio kivitendo ngoja niwakumbushe wasomaji wangu wengi wetu tunamfahamu hashim  thabit anayecheza mpira wa kikapu marekani mpaka anafika alipo sasa ni jitihada binafsi kwa aslimia themanini hakuna mchango wa wizara hata kidogo mara kadhaa timu mbalimbali za michezo husika zimekuwa zikikosa hata nauli ya kwenda kwenye mashindano na kuanza kuomba misaada hii ni fedheha na aibu kwa wizara na serikali ,wapo viongozi  wa vyama vya michezo wanalalamika hawana fedha lakini wizra imekaa kimya.

Mh Leornad Tadeo unataka akutunzie nani vijana hao wa airtel rising star kama ulikuwa unajua kuwa hawana mwenendelezo mzuri kwanini ulikwenda kuzindua mradi ule pengine Tadeo atueleze kuwa kazi yake hasa nini akiwa kama mkurugenzi wa michezo au atuambie kazi ya wizar yake  nini ni? kama serkali imeweza kujenga kiwanja cha soka inashindwaje kujenga shule ya serikali tena ya michezo kwakweli  kwa kauli ya Mh Tadeo Tanzania haitaweza kufuzu kombe la dunia kamwe kwani haiwezekani mkurugenzi wa michezo usijue kinachoondelea katika wizara yake ili ni jambo la kuustaajabisha kabisa hatutaweza kufikiri siku moja kuwa Mtu mkubwa kama huyu angeweza kuuliza jambo la kama hili hadharani kiasi kile !
Lakini sasa hatushangai tena kwa sababu ukitazama viwanja vyote ambavyo vinamilikiwa na selikari ukiacha uwanja mpya na ule wa uhuru , vingine vyote ni hohe hahe havifai na hivi viwli vya Dar es salaam vimekuwa vikikarabatiwa kwa sababu mara kadhaa vimekuwa vikitumiwa na serkali kwa hafla mbalimbali .

Airttel Rising star ushirikiana na klabu ya Manchester united katika ukuzaji vipaji hata kama watafudhu ni vigumu kwa kundi lote lile kwenda manchester kufunzwa soka mawazo yetu yalikuwa serikali na tff ikishirkiana na Airtel kutengeneza au kujenga shule kubwa ya michezo .na  bila kufanya hivyo Mkurugenzi wa wizara ya habari utamaduni na michezo Ataendelea kujiuliza swari ambalo yeye ndiye muwajibikaji 
Tadeo umewashangaza wanamichezo. !!!!!    

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers