HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

24 May 2013

NI SIMANZI TUPU UMISETA MBEYA

Baadhi ya viongozi na wanafunzi walisimama dakika moja kumwombea marehemu
Afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amemtaja marehemu kuwa mtu aliyekuwa na mchango mkubwa katika ufundishaji wa somo la hisabati shuleni hapo na pia usimamizi wa shughuli za michezo.
Afisa michezo mkoani hapa George Mbijima amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwalimu Chalo kwakuwa kilitokea ikiwa ni muda mfupi umepita tangu walipokuwa katika kikao cha pamoja kabla hajawaacha na kwenda kushughulikia shughuli ya ugawaji chakula kwa washiriki wa mashindano na kisha kuanza safari kurudi nyumbani kwake.
Baadhi ya wanafunzi washiriki wa mashindano ya wanafunzi wa shule za sekondari(UMISETA) mkoani Mbeya yanayoendelea katika viwanja vya Sekondari ya Iyunga pamoja na Viongozi wakifuatilia hotuba ya afisa elimu mkoani hapo Mwalimu Juma Kaponda kabla ya kufungua mashindano hayo leo.



MASHINDANO ya wanafunzi wa shule za sekondari(UMISETA) mkoani Mbeya yamefunguliwa kwa simanzi kubwa baada ya mmoja wa waratibu wa mashindano hayo kupoteza maisha katika ajali. Aliyepoteza maisha usiku wa kuamkia leo ikiwa ni siku moja baada ya kuanza kwa mashindano hayo ni mwalimu Abdalah Chalo(41) wa shule ya sekondari Iyunga ya jijini hapa aliyegongwa na lori wakati akiendesha pikipiki alipokuwa akirudi nyumbani kwake muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kugawa chakula kwa washiriki wa michezo. 

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman mwalimu Chalo aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba T 815 BKQ aina ya King Fan alikutwa na mauti baada ya kugongwa na lori lenye namba T 441 BYW aina ya Scania likiwa na tela lenye namba T 496 BWD. Kamanda Athuman amesema tukio hilo lilitokea Mei 22 majira ya saa 3:00 ya usiku katika eneo la Iyunga darajani jirani na nyumbani kwa marehemu na kumtaja dereva wa lori kuwa ni Heri Faustin(35) mkazi wa eneo la Mama John jijini Mbeya.

 Akifungua mashindano ya Umiseta alhamisi hii katika viwanja vya shule ya sekondari Iyunga,afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amemtaja marehemu kuwa mtu aliyekuwa na mchango mkubwa katika ufundishaji wa somo la hisabati shuleni hapo na pia usimamizi wa shughuli za michezo.

 Naye afisa michezo mkoani hapa George Mbijima amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwalimu Chalo kwakuwa kilitokea ikiwa ni muda mfupi umepita tangu walipokuwa katika kikao cha pamoja kabla hajawaacha na kwenda kushughulikia shughuli ya ugawaji chakula kwa washiriki wa mashindano na kisha kuanza safari kurudi nyumbani kwake.

 Mashindano ya Umiseta kwa mkoa wa Mbeya mwaka huu yanashirikisha jumla ya wanafunzi 1 kutoka halmashauri 1066 za mkoani hapa lengo likiwa ni kupata wanafunzi 125 watakaounda timu ya mkoa kwaajili ya kushiriki mashindano hayo katika ngazi ya kanda.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers