HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

31 May 2013

RAIS LYDIA NSEKERA AVUNJA REKODI YA MIAKA 109 FIFA

Lydia Nsekera


Rais wa chama cha soka cha Burundi FA  Lydia Nsekera amechaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza katika kamati kuu ya fifa na kuvunja rekodi ya miaka 109 .
Nsekera, 46, atahudumu kwa miaka minne baada ya kushinda katika kura zilizopigwa  katika mkutano mkuu wa fifa  huko  Mauritius.
Nsekera alikusanya kura  95 kati ya mia mbili na tatu  203 akiwazidi kete wakuu wa soka la  Australian Moya Dodd na  Sonia Bien-Aime, kutoka Uturuki  na visiwa vya  Caicos.
Nsekera anasema : "Nitawachagiza wanawake waamini kuwa wanaweza kuongoza na nitawaunga mkono wanawake wote katika vyama vya soka ."
Nsekera,ambaye mwaka jana alipendekezwa kuchaguliwa kugombea katika kamati kuu ,ameliongoza shirikilisho la soka la Burundi Tangu  2004 na alikuwa mwanachama kamati ya maandalizi ya mashindano ya 2008 na  2012 .
akiwa kama mwanachama wa maandalizi ya olimpick pia alikuwa katika kamati huru ya  kuzuia rushwa mwaka 2011 .
Nsekera ameimbia  BBC: "Ninafuraha sana kuwa mwanamke wa kwanza  ni jambo muhimu kwa afrika na ni muhimum pia kwa Burundi na kwa wanawake pia .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers