HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

21 May 2013

SAM TIMBE KUKAA BENCHI MOJA NA MICHO UGANDA CRANES

 
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda  Milutin “Micho” Sredojević amechaguliwa kuwa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya uganda akiziba nafasi ya  MScottish Bobby Williamson ambaye aliachishwa kazi  mwezi jana
Micho ambaye ni Raia wa  Serbian amechaguliwa mchana wa leo katika makao makuu ya Shirkisho la soka la uganda  (Fufa House) huko Mengo,kilometa chache kutoka  jiji la  Kampala . na ametia saini kandarasi ya miaka miwili .
Williamson aliiongoza Uganda Cranes kushinda mara nne kombe la baraza la vyama vya soka la afrika mashariki na kati  Challenge Cup lakini alishindwa kuipeleka ti mu hiyo katika mashindano ya mataifa ya afrika .
Aidha  Micho amesema na akitumia Lugha ya kiganda kwa lafudhi mbaya "  Luganda ,  “Naskia heshima sana na kujivunia kupewa kuifundisha timu ya taifa ya Uganda ambaye aliiondoka uganda 2004, nilikuwa sipo kimwili lakini roho yangu ilikuwa hapa na inapendeza sana kurudi hapa. Na nina imani kuipeleka nchi mbali zaidi ” 
Micho, 43, atasaidiwa na kocha wa timu ya  polisi ya uganda  Sam Timbe, na kocha wa Bul Bidco  Kefa Kisala na  kipa wa makocha  Fred Kajoba.
Aidha kocha huyo amewahi kufundisha timu za St.George of Ethiopia, South Africa’s Orlando Pirates pia  Al Hilal ya Sudan

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers