HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

18 May 2013

SIMBA KAPAKATWA JANGWANI

 
Klabu ya soka Yanga ambao  ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara wamewakandamiza watani wao wa jadi simba kwa mabao mawili kwa sifuri katika mchezo uliohudhuliwa na mashabiki Hamsini na saba elfu mia nane ishirini na tano mchezo ambao uliamuliwa na mwamuzi Martin saanya kutoka Morogoro ambaye pia ni Askari Magereza .

Yanga hawakuchukua muda kuwaonyesha watani zao kile kilichowafanya wao kwenda pemba kwani katika dakika ya tano ya mchezo Didier Kavumbagu aliunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Haruna niyonzima "Fabregas"na kuipachikia Yanga bao la kuongoza na kuufanya umati wa watu kulipuka kiwanjani hapo.
_MG_0398
PICHA NI KWA HISABI YA FULLSHANGWEBLOG wachezaji wa yanga wakiwa wanashangalia bao la kwanza

katika dakika ya ishirini nane mrisho ngasa alifanyiwa faulo katika kisanduku cha yanga na hivyo mwamuzi Martin saanya kuizawadiwa simba Mkwaju wa penati lakini Musa mude aliyepewa jukumu la kupiga penati hiyo alikosa baada mlinda mlango wa yanga ally Mustafa Barthez kudaka penati hiyo mpaka kipindi cha kwanza   yanga ilikuwa inaoongoza goli moja kwa sifuri .

Kipindi cha pili simba ilifanya mabadaliko Abdalah seseme alikwenda nje na kuingia Felix Sunzu lakini mabadailiko hayo hayakusaidia chochote kwani yanga ilipata bao la pili katika dakika ya 63 Mbuyu Twite alirusha mpira mithiri ya kona ambao uliwagonga baadhi ya wachezaji wa simba na kumkuta Hamisi kiiza Diego na kufunga goli zuri kwa lugha ya kiingereza huitwa Voley goli lilowazima kabisa mashabiki wa simba na kuwafanya mashabiki wa yanga kuanza kejeri na kuonyesha alama ya kisu shingoni wakiwa na maana mnyama kauwawa .
_MG_0401
Wachezaji wa yanga wakiwa na furaha baada ya kuifunga simba leo katika uwanja wa taifa PICHA NA FUULSHNGWEBLOG.
kadri muda ulivyozidi kwenda mbele simba ilionekana kuja mchezo  lakini Amri Kiemba ,mwinyi kazimoto, hawakuweza kufua dafu leo hii na hata walipo jaribu kupiga mashuti yaliishia mikononi mwa ALLY MUSTAFA mlinda mlango wa yanga katika dakika za mwisho Nizar khalafan akichukua nafasi ya Hamis kiiza alipiga kombora baada ya mchezaji wa yanga kufanyiwa wa faulo mita takriban ishirini na tano mpira huo uligonga mlingoti na kugonga kichwani mwa mlinda mlango wa timu ya simba Juma kaseja na kumfanya kupoteza fahamu kwa dakika chache  lakini mchezaji huyo alirejea kiwanjani kama kawaida .
Lakini katika hari isiyokuwa ya kutegemewa na kutofahamika mwamuzi martin saanya alijeruliwa jicho la kushoto na kuvuja damu lakini haikufahamika nani aliyemjeruhi kati ya mchezaji  wa yanga au simba.

_MG_0384
Mchezaji wa timu ya Yanga Didier Kavumbagu akikokota mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Simba Abdallah Seseme katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom unaofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam , hivi sasi ni kipindi cha pili na Yanga wanaongoza magoli 2 -0 dhidi ya Simba ambayo imekosa penati katika kipindi cha kwanza wakati mchezaji wake Mussa Mude akipiga vibaya mpira huo baada ya Mrisho Ngassa wa Simba kuangushwa kenye eneo la hatari PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWEBLOG
Kwa maana hiyo  yanga wanafikisha alama sitini 60 huku azam ambao wameifunga Oljoro jkt mabao mawili kwa moja katika mchezo uliochezwa katika uwanja sheikh amri abeid kaluta huko Arusha wanafikisha alama hamsini na nne simba wanabaki nafasi ya tatu wakiwa na alama zao 45 wakicheza michezo ishirini na sita baada ya kufungwa na yanga mabao mawli kwa bila matokeo mengine leo hii
JKT RUVU 1MTIBWA O
KAGERA SUGAR 1TZ PRISON 0
TOTO AFRICAN2 RUVU SHOOTING 0
AZAN 2OLJORO JKT 0
        

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers