FIFA World Cup tickets to go on sale
© Getty Images
Wakati mechi za kufuzu kushiriki kombe la dunia zikiwa zimeshika hatamu kila pahala katika mabala yote katika kuelekea mwaka  2014 ™ na kuitafuta timu ya kwanza kufuzu mashindano hayo ili kwenda kumenyana na magwiji wengine huku katika bara la Asia  kukiwa kumesalia mechi moja ya kuamua timu ya kwanza kwenda Brazil .
Mashabiki wa soka wanasubiri kwa hamu kubwa siku ya ufunguzi wa kuanza kununua tikiti hizo ,katika mashindano ambayo yataanza  katika miji  12 huko  Brazil kuanzia 12 June hadi  13 July 2014.
Kwani Tarehe 20 August 2013,mashabiki wa soka duniani kote watapata nafasi ya kuomba kununua tikiti kupitia mtandao wa FIFA  www.FIFA.com.kuhusu bei ya tikiti na maelekezo mengine yatapatikana kwenye tovuti hizo  kuanzia  1 July 2013.