HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 June 2013

MBUZI WAINGIZA MILIONI 130 DAR ES SALAAM !!!!



Hakika, MBUZI MMOJA TU anaweza Kufanya Mabadiliko!

Mbio za Hisani za Mbuzi za Dar 2013 zimeweka rekodi kwa kufanikiwa kukusanya Shilingi milioni 130 zitakazosaidia mashirika mbalimbali ya hisani ya ndani ya nchi, imeelezwa na waandaaji leo. 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitDdEUko2SVegpCuQxJl3156TPDII-I7twmZyULKt3vUMn0BYgDU0YgfVkpMBTooRfCDOPsOid2MLY1XgLmhFe28EeloljHEhwcnwLqZXso9yxbAiVIMnCoPEF8Q3-JkUzQDJPl14N5Dg/s1600/GOAT+01.JPG Kwa maana hiyo basi, hadi sasa mbio hizo zilizoanza tangu mwaka 2001, zimekwishakusanya zaidi ya Shilingi milioni 790 kwa ajili ya mashiriki zaidi ya 60 ya hisani.

Takribani watu 4,700 waliingia getini ili kushuhudia mashindano ya 13 ya Mbio za Mbuzi za Hisani katika Viwanja vya The Green, Kenyatta Drive jijini Dar es Salaam siku ya Juni 1 mwaka huu. 


Mwenyekiti wa Kamati ya Mbio za Mbuzi, Karen Stanley alisema: “Tuna furaha kubwa sana kutangaza kuwa kwa mara nyingine mwaka huu pia tumefanikiwa kukusanya fedha nyingi kuliko hata mwaka jana baada ya kupata Shilingi milioni 130 kwa ajili ya mashirika yaliyochaguliwa.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRSxDwST-nuDvPdVdlAQxnfOr07D14F6dn4RvgsK1T9uE6BRba4_ZEFszg2CYhLOmKF18O2z7UFdo1mgqKAJd4cwvtqAgO34qF7GjBlkX9hhbGKLGBmfhSeme-rIVpLc70FTeUsyShSk0/s1600/goat+02.JPG“Shukrani ziwaendee watu 4,700 waliofika kushuhudia tukio hilo kwa mwaka huu, na sasa tunaweza kusema kwamba tumeongeza idadi ya mashirika yatakayonufaika kwa makusanyo hayo mwaka 2013 kutoka tisa ya awali hadi 16. Miongoni mwa mashirika hayo, yapo yale ambayo yamekuwa yakinufaika kila mwaka lakini pia yapo mapya. 

 “Fedha zinazokusanywa kutokana na mashindano ya Mbio za Mbuzi huleta mabadiliko kwenye mashirika madogo madogo ya hisani yasiyo na fursa pana za kupata fedha nyingi. Mbali na furaha na burudani zinazopatikana siku ya tukio, kitu kikubwa katika mbio hizi ni kusaidia vikundi na mashirika haya ya hisani yanayopambana kuyabadili maisha ya mtu mmoja mmoja.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8Ce0y7QYBrEHbfAli7t4d4pCoTCUqJRkCaO3fm8f2uVRGtyvZXFaZbOfe96jiQpX3ERFnpWcG-JIDQkwPArqLU5Hu7mzqKHDNdam_RsAdaskt9oqkE4qgwosSjTO59_pvHzlT5SyB8Co/s1600/goat+03.JPG“Tunawashukuru maelfu ya watu walioshiriki, wakatuunga mkono na kuja kwenye tukio hili la burudani, pamoja na wafadhili kwa moyo wao wa ukarimu na kujitoa kwani bila wao haya yote yasingefanikiwa.”

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu www.goatraces.com




: Mwenyekiti wa Kamati ya  Mbio za mbuzi za Hisani Dar es Salaam, Karen Stanley (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 35 kwa Boniventure Mchovu zitakazopewa kwa mashirika ya kujitolea 16 ambazozilipatikana wakati wa mashindano ya bio za mbuzi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 1 Mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyikan jijini Dar es Salaam



Mwenyekiti wa Kamati ya  Mbio za mbuzi za Hisani Dar es Salaam, Karen Stanley (katikati aliyevaa gauni jekundu) akipozi kwa picha pamoja na baadhi ya wadhamini na wawakilishi wa mashirika ya hisani 16 katika hafla ya kuyakabidhi mashirika hayo shs milioni 35 zilizopatikana wakati wa mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyikajijini Dar es Salaam Juni 1 Mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyikan jijini Dar es Salaam



Wasanii wa kikundi cha Kigamboni Community Centre wakitoa burudani katika hafla ya kuvikabidhi vikundi 16 vya hisani msaada wa fedha wa shs milioni 35 zilizopatikana wakati wa mashindano ya mbio za mbuzi ya mwaka huu. Hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam





 Mashirika yanayonufaika mwaka huu:






Matumaini Day Care Center for Disabled
Children – www.holyuniontanzania.co.ok

Zanzibar Outreach Program (ZOP) – www.zopzanzibar.org
Bibi Jann's Centre – www.bibijann.org
Fahari Zanzibar – www.fahari-zanzibar.com
CCBRT (Comprehensive Community Based
Rehabilitation in Tanzania) -  www.ccbrt.org.tz

Malaika Kids –  www.malaika-kids.net
AC-AF – www.ac-af.com
Foxes'
Community and Wildlife Conservation Trust – www.foxesngo.org

The Daughters of Mary Immaculate and
Collaborators (DMI) - www.dmimissionafrica.org

Sea Sense – www.seasense.org
Ramat – www.ramat-tz.org
Wonder Workshop – www.wonderwelders.org
Molly’s Network – www.mollysnetwork.org
Kidzcare Kerege Children’s Home and Pre-School
friends@cats-net.com

St Paul’s English Medium Primary School – Wilfred_muhogolo@yahoo.com
The Mango Tree Orphan Trust – www.themangotree.org

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers