HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 June 2013

SIMBA MNAMATATIZO GANI NA MAKOCHA WAGENI ?


 http://2.bp.blogspot.com/-z6HdZHKFG18/Ubn7daJC8gI/AAAAAAAEdTk/va2apLIGPS8/s1600/images.jpg


Aliyekuwa kocha Simba Patrick Liewig (pichani) amerejea nchini na kuitaka klabu hiyo imlipe malimbikizo ya mshahara wake kisha iachane naye kwa amani. Simba iliachana na  Liewig baada ya kutoridhishwa na matokeo ya mechi za msimu uliopita na kuishia kukamata nafasi  tatu.

Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana alfajiri,Liewig alisema,hawezi kulazimisha Simba imwongezee mkataba  isipokuwa anachohitaji ni malipo ya malimbikizo ya mishahara yake.

"Nimekuja hapa kwaajili ya kutaka kujua kinachoendelea, sababu nimesikia tu  juu juu kuwa sitakiwi kwenye timu na sijaambiwa rasmi.

"Pamoja na hayo mimi sina tatizo,kama wameamua hivyo kuachana na mimi sawa isipokuwa wanilipe fedha zangu ninazodai kwani ni haki yangu na ndio maana nimekuja Tanzania"alisema Liewig

Aliongeza" Mkataba wangu umeisha Juni lakini kuna fedha zangu bado nawadai hivyo siwezi kuziacha hivi hivi, lazima wanilipe ndipo tumalizane kwa amani".

Kocha huyo aliichukua Simba mikononi mwa kocha aliyetimuliwa Milovan Cirkovic na alianza kuinoa timu hiyo kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo alisifika kwa ukali wake kwa wachezaji na hivyo kuamua kufanya uamuzi mgumu wa kuwasimamisha baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo kwa madai ya utovu wa nidhamu na kuwatumia vijana katika michezo  10.

Hata hivyo habari za ndani zinadai kuwa kocha huyo anaidai klabu hiyo malimbikizi ya mshahara wa miezi mitatu unaofikia kiasi cha dola 36,000.

Kaimu Makamu mwenyekiti wa Simba Joseph Itangare alisema hawana taarifa ya ujio wa kocha huyo lakini wanasubiri kama atawasiliana nao basi watamsikiliza.

"Sisi hatujui kama amefika hapa nchini lakini tunangoja kama atawasiliana na sisi tutafanya mazungumzo naye" alisema.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers