HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 June 2013

Rio Ferdinand AWAAMBIA ,Cesc Fabregas NA Robert Lewandowski WATAKUWA VICHAA WAKIACHA KUSAINI MAN U

Ferdinand

Rio Ferdinand Amewaambia wachezaji wanao tafutwa kwa udi na uvumba  na Man u  ,Cesc Fabregas na  Robert Lewandowski watakuwa wachezaji wazuri kama watachezea  Manchester United
Beki huyo wa zamani wa Uingereza  amesema kuwa hakuna sehemu ambayo mchezaji anaweza kuwa Bora na kufanikiwa kwa vitu vingi zaidi ya kuchezea klabu hiyo  kama alivyofanya winga  Cristiano Ronaldo .

Fabregas, 26, na  Lewandowski, 24, wapo katika orodha ya kocha mpya wa  United’ David Moyes ambaye ana lengo la kuubakisha  ubingwa wa ligi ya uingereza.

Kama  United ikikuhitaji , unatakiwa kukubali.,’ Ferdinand, 34, aliliambia  The Sun.
Hata kama ukiwa mchezaji mkubwa lakini unakuwa mzuri ukiwa hapa . Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji bora akitokea Sporting Lisbon.
‘Kama ilivyokuwa kwa Ryan Giggs, Roy Keane, David Beckham, Andy Cole ambao wamekuwa wachezaji bora wakiwa United.kwa  hari hii huwezi kuamini kama kuna mtu atakataa kuja kucheza hapa  .
'Ukiwa na ndoto za kutaka kuteng'eneza jina lako .Na ukiwa Mchezaji Mwenye umri wa miaka   23 na  27 hicho ndicho kitu ambacho unaweza kukitaka na utaonekana unakwenda sehemu ambayo unahitaji kutwaa vikombe .'

Mshambuliaji kutoka Poland Lewandowski alikuwa na ndoto za kwenda kuchezea ' Bayern Munich lakini ndoto hizo zimezimwa , lakini  Dortmund wanaonekana ni bora wamuuze katika klabu ambayo itayokuwa nje ya nchi hiyo ambapo kandarasi yake inakaribia kwisha mwakani ,huku mchezaji wa zamani  na nahodha wa timu ya Arsenal  Fabregas amehusishwa na kurejea katika ligi kuu ya buingereza baada ya kushindwa kupata namba ya kudumu akiwa Barcelona.
Moyes anaonekana kutaka kuziba nafasi mshambuliaji ambaye hajatulia Rooney na nafasi kiungo bora kabisa katika jiji la Manchester  Paul Scholes.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers