HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

1 June 2013

YANGA KUJIFUA LOYOLA KATIKA MAANDALIZI YA KAGEAME


 

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara 2012/2013 Young Africans  ambao pia ni Mabingwa watetezi wa kombe la Kagame. jumatatu wanatarajia kuanza mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola Mabibo kujiandaa na mashindano ya kombe la Kagame yanayotarajia kuanza Juni 18 mwaka huu nchini Sudan.
Katika mashidano ya mwaka huu nchini Sudan , Yanga imepangwa katika kundi C lenye timu za Express FC (Uganda), Vitaloo FC (Burundi) na Ports FC (Djibout) ambapo kundi hili litakua katika mji wa El Fashir Kaskazini mwa jimbo la Darfur. 
Yanga itaanza kutetea ubingwa wake Juni 20 dhidi ya timu ya Express ya Uganda, kisha Juni 22 itacheza na Ports ya Djibout kabla ya kumalizia mchezo wake wa mwisho katika makundi dhidi ya timu ya Vitaloo Juni 25 michezo yote ikifanyika katika uwanja wa El Fashir.
Mpaka sasa klabu ya Yanga imefanikiwa kukamalisha usajili wa mchezaji Mrisho Ngasa aliyekuwa akiitumikia Simba SC kwa mkopo akitokea timu ya Azam Fc ambapo mara baada ya msimu kumalizika amejiunga Yanga kama mchezaji huru. 
Mara baada ya mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba Kocha Mkuu Ernie Brandts alitoa mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya kupata nafasi ya kujumuika na familia zao, ndugu zao kabla ya kurejea June 3 na kuanza maandilizi ya mashaindano hayo. 
Young Africans ambayo ilitwaa ubingwa wa VPL ikiwa na michezo miwili mikononi inaanza mazoezi jumatatu asubuhi kuhakikisha inajiandaa vema kwenda kushindana na kurudi na kombe hilo kwa kulitwaa kwa mara ya tatu (3) mfululizo, ambapo mpaka sasa imeshalitwaa mara 5.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers