HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

23 July 2013

LIGI KUU BARA ,KELELE,VISINGIZIO NA MPIRA WA MDOMONI ,KUREJEA UPYA .


Ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo inatarajia kuanza August 24 Kwa timu zote kuingia kiwanjani huku baadhi ya timu zikiwa zimepanda na nyingine kushuka wakati Bingwa Mtetezi Ni Dar Es Salamm Young afrika huku Azam fc ikiwa imeshika nafasi ya pili katika ligi iliyomalizika mismu uliopita.

Lakini ligi hii itaanza hivi karibuni pengine inaweza kuwa Kero au Karaha kwa wapenzi wa soka la Tanzania kwani ule muda wa visingizo vya maandalizi mabovu umewadia ,Refa hafai, Ratiba ina upendeleo kwa timu kadhaa mapato madogo ,pingamizi za wachezaji Tulisahau kama ana kadi tatu za njano , Kocha hafai na mengine mengi utayapata kupitia vyombo vya habari pale baadhi ya mashabiki na makocha na wasemaji wa timu watakapokuwa wakitoa sababu za wao kufungwa au kupoteza mchezo wowote wa ligi hata kama timu yao haina uwezo .

Kwa mimi Binafsi sishangai sembuse na ligi yenyewe hatuioni mpaka Super Weekend ambayo bado hatujawa na uhakika wa huduma hiyo kama msimu huu itakuwepo tena au itaboreshwa zaidi.

Alama yangu ya msingi Timu zetu za Tanzania ni timu ambazo tayari zinakuwa zinajiandaa kwa kila kitu yaani kimchezo na Visingizio vya kufungwa, lakini kwa miaka kumi ambayo tumekuwa tukishuhudia Ligi ya Bara hakuna siku ambayo huwa hakuna visingizo ni mara moja moja sana utakuta timu zinakubali kilichotokea uwanjani .

Sitaki kutoa mifano ya ligi za ulaya kwenye ligi yetu kwani sioni pa kuweka mfano huo kwa lugha ya kimombo Doesn't Apply kwani wameanza kuona mpira  siku nyingi katika Runinga na wamekuwa wakisifia sana cha ajabu wameshindwa kuiga yafutayo Ustaalabu mashabiki wachezaji pamoja na viongozi .
,Elimu,Uendeshaji,Uanamichezo,Haki za Televisheni 

Najua hatukosi kujitetea wametuzidi maendeleo lakini nchi nyingine hapa afrika tumezisaidia hata kugombania Uhuru iweje zitupite kisoka haina haja kuzitaja maana ni aibu na kufedheheshana kila mwaka huwa tunasema kuwa tujifunze ligi iwe nzuri hakuna asiyependa hilo lakini tunaanzia wapi kujifunza kuna maswali ya kujiuliza na la msingi kuna baadhi ya mambo hayaendeshwi na Maskini hata siku moja kwa mfano mpira wa leo hauwezi kundeshwa na watu maskini kwani unahitaji gharama sana .

Jambo moja kuu na la msingi mambo mengi ambayo uanzisha kelele kwa soka Ni pesa mapato ya viwanjani kama simba na yanga zitakuwa zinalia wakati huo huo zinatumia mamilioni ya shilingi kuchukua magarasa kutoka Nigeria,Ghana,Cameroun bila kusahau mipango Finyu ya vyanzo vya mapato na mambo mengi sana ya kiutawara unajua inaweza isikuingie akilini huwa nafikilia sana lini Tanzania itafikia heshima walioyopata wakina Tenga kule Nigeria jibu la haraka :- Ni ndoto Pengine ni rahisi zaidi kwa Ngamia kupenya katika Tundu la sindano kuliko kuuleta siku moja ubingwa wa afrika kama sio shirikisho Tanzania.

Jamani tunashindwa nini kubadilika sitaki kuamini kuwa Tumelaaniwa kiasi hicho au soja sio fani yetu 

Nadiriki tena kusema timu pekee ambayo itakuja kuibeba Tanzania Katika mashindano ya kimataifa Ni Azam fv ambayo kama watafuata miiko soka itakuwa bora kuliko Tp Mazembe .    

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers