HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 July 2013

Omari Kimweri 'Lion Boy 'ACHAKAZA WAZUNGU ULAYA !

Omari Kimweri
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri  'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini   Australia amendelea kutamba katika nchi hiyo baada ya jana kumtwanga kwa  KO ya raundi ya kwanza bondia Ekkalak Saenchan wa Thailand   ikiwa ni mchezo wake wa 16 tangia angie katika ngumi za kulipwa akiwa nchini humo 
Bondia huyo ambaye anaitangaza vema nchi ya Tanzania Kimataifa ameaidi kuwa ataenderea kutoa vipigo kwa mabondia  mbalimbali  pindi wakutanapo ulingoni 
Bondia huyo aliezaliwa Tanzania katika jiji la Dar es salaam mwaka 1982 amekuwa gumzo nchini humo kwa kuonesha mchezo mzuri unaowavutia raia wengi wa Australia na kuweza kuwa bondia namba moja katika nchi hiyo uku katika Dunia akishikilia nafasi ya 52 katika mabondia 450 duniani wenye uzito wa light flyweight


Anasema lengo lake kubwa ni kuukamata ubingwa unaotambulika kimataifa Duniani wa WBA World light flyweight title unaoshikiliwa na bingwa namba moja Duniani ,Roman Gonzalez na IBF light flyweight title   unaoshikiliwa na  John Riel Casimero wa  Philippines ambao wananiumiza kichwa kwa sasa kwani ngumi ulimwengu mzima ni zile zile ila tunazidiana maarifa

Bondia huyo anaefanya shughuli zake za masumbwi nchini Australia ana mpango wa kuja kuwekeza nchini Tanzania mchezo wa masumbwi ili ukuwe hapa ambapo atafanya kila jitiadi ili mchezo wa masumbwi uweze kusonga mbele nchini habari hizi kwa ushirikiano mkubwa wa mtandao wa www.superdboxingcoach.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers