HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 August 2013

Ian Wright :SUAREZ KHERI UBAKI LIVERPOOL LAKINI SIO KWENDA ARSENAL


Luis Suarez Anatakiwa kubaki Liverpool na kutupilia mbali offa ya kwenda kucheza katika klabu ya Arsenal, Hii ni kauli ya Mchezaji na mshambuliaji wa zamani wa washika Bunduki  Ian Wright.


Liverpool imekataa offa mbili zilizotolewa na klabu ya  Arsenal kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka  26-, ambaye anataka kucheza ligi ya mabingwa ulaya.

"Nitamkaribisha  Arsenal kwa mikono  yangu yote miwili," Wright ainaiambia BBC Sport.
"Lakini ningekuwa  Suarez, na ukitazama vitu vyote pale,Haionyeshi kama kuna jambo la umuhimu wa yeye kwenda Arsenal. Ningempa nafasi moja zaidi kubaki  Liverpool ."

Wright, ni moja kati ya watangazaji wa kipindi cha mpira wa miguu  cha BBC Radio 5 live's sambamba na  Kelly Cates, anaongeza : "Arsenal sasa imeamua kuamka na kushindania majina makubwa na bila kufanya hivyo itaachwa nyuma."

Mshambuliaji huyo amesha sema kuwa Angependa kuondoka Anfield japokuwa amesaini kandarasai ndefu mwaka 2012 Mwezi  August .

Anaamini kuwa offa ya karibuni iliyotolewa na  Arsenal's ya pauni £40m jumlisha  £1 kama ushawishi inamrushusu yeye kuanza kuongea na klabu nyingine,Lakini Liverpool aionyeshi kuwa wanataka kumuuuza mchezaji huyo mpaka itakapo fika kitita cha £50m-.


Huku Liverpool ikiwa haijacheza michuano ya Ligi ya mabingwa Barani ulaya Tangu  2009, Arsenal itakuwa inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kumi na saba mfululizo .

 Wright anadhani kuwa hata kama wakimleta  Suarez, Bado majina makubwa yanahitaji kuletwa .
"Tunahitaji kuona mambo ambayo hatujayaona kwa muda mrefu kidogo na wanatakiwa kufanya hivyo kama wanavyofanya  Manchester United, Manchester City , Chelsea ," .

"Lakini sidhani kama wako ndani ya wakati kwa sababu , kwa sasa,wanahitaji kufanya kazi ya ziada kwa hawajashinda kitu chochote kwa muda mrefu .Hii ndio sababu Arsenal  kuwa katika hari ya hatari.


"Ningependa kuwaona wakienda mbali zaidi kuhusu  Suarez, lakini hawawezi tu kumnunua yeye na timu nzima kubaki vile vile . Nadhani wanahitaji Mlinda Mlango ,Walizini wawili wa kati, walinzi wa kulia na kushoto   - Viungo wengine na washambulizi wawili.

" Haita leta maana kwa kumsainisha Suarez kwa pesa hiyo na kuacha kufanyika marekebisho nafasi nyingine  ."

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers