HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

1 September 2013

PESA SIO KILA KITU KASKAZINI MWA LONDON ,STURRIDGE AKATA KEKI YA 24 ANFIELD ?

Arsenal v Tottenham
Arsenal imeendelea kurejesha Heshima katika dimba la nyumbani baada ya kuiibamiza  Tottenham kwa goli moja kwa sifuri goli lililowekwa kimiani na Olivier Giroud na kuifanya Spurs kupata Kipigo cha kwanza msimu huu  . 

Olivier Giroud amefunga goli lake la nne msimu huu baada ya kuunganisha mpira kwa mguu wa kushoto yaani auta krosi iliyo pigwa na Theo Walcott's na kutumbukiza mpira kwenye Nyavu Ndogo .
Andros Townsend alipiga shuti ambalo liliokolewa na mlinda mlango wa Arsenal ,Huku Hugo Lloris akiwabania   Giroud na Walcott baada mapumziko.
Wojciech Szczesny alizuia bakola ya  Jermain Defoe's ambayo ilikinzwa na kuifanya arsenal kushika nafasi ya nne katika ligi ya uingereza .
Lakini mashabiki wa Arsenal waliingiwa na mashaka baada ya kiungo wao  Jack Wilshere kutolewa kabla ya nusu ya mchezo kuisha lakini Arsene Wenger anasema kuwa ni uchovu na sio majeraha . 
Olivier Giroud
.
Villas-Boas ametumia Pauni mil  £107m kusajiri wachezaji wapya wakai huu wa kiangazi lakini huku wachezaji wake wakionekana kuwa ni bora ,Walionekana kuwa hawana kasi dhidi ya Arsenal ambayo ina wachezaji wengi wenye uzoefu katika ligi ya  uingereza   -na wanaonekana watakuwa na nyakati ngumu zaidi pale  Gareth Bale,atakapo maliza uhamisho wake kwenda Real Madrid.
DANIEL STURRIDGE 1- MANU 0
Daniel Sturridge 
Liverpool imejikita kileleni baada ya kuanza vizuri katika msimu huu tangu ilipofanya hivyo mwaka  1994-95 ilipopata ushindi dhidi ya Bingwa Mtetezi  Manchester United pale  Anfield.
Daniel Sturridge alisherekea sikukuu yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka   24th Akiwa anaipatia Timu yake ushindi wa tatu mfululizo baada ya kufunga goli la kwa kuupalaza mpira kwa nyuma na kutinga wavuni katika dakika ya Tatu.
Liverpool inastahili ushindi kwa aina yao ya ushindi wa goli moja kwa bila na kuandika Takwimu Mpya ya ushindi wa Goli moja kila mechi Na mfungaji akiwa ni yule yule na kumfanya David Moyes' apaone pachungu Anfield . 

Mechi nyingine Swansea 2-0WBA 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers