HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

4 September 2013

TFF NA ZFA REJESHENI LIGI YA MUUNGANO WACHEZAJI WAPATE KUFAHAMIANA !

Wiki nilipata Kutazama kituo kimoja cha Televisheni Cha Jijini Dar Es salaam Maarufu kama Channel Ten ambapo walialikwa wachezajhi wawili wa Timu Yanga na KMKM Lawrence Mwalusako na Abdalah Maulid walikuwa wakizungumzia kuhusu Tamsha la Miaka Hamsini ya kusherekea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Tangu ijikomboe kwa Utawala wa Sultan .

Leo nimeona Bora nilizungumze jambo hili kiundani kidogo moja kati ya mambo yaliyokuwa yakizungumzwa Nilifurahishwa sana Na Abdallah Maulid ambaye hakuficha aliweka wazi kuhusu aonavyo jambo la Muungano katika michezo Binafsi yangu ninakubali yote aliyoyazungumza kwani ukiyatazama kwa upana wake ya na maana kubwa sana katika mboni ya soka katika siku za mbele .

Abdallah yeye alikwenda mbali zaidi kwa kuizungumzia Nchi yake ya moyoni kwa kusema kuwa tangu ligi ya Muungano iyondolewe timu za Zanzibar zimeshuka kiwango sana kutokana na kuwa hazipati changamoto kutoka timu za Bara kwani Bara kuna timu nyingi zaidi kuliko Zanzibar jambo linazifanya timu za Zanzibar kukosa uimara na kukosa changamoto  .

Jambo kuu kubwa ambalo nadiriki kukubaliana nae wazi wazi ni kuwa wachezaji wa Zanzibar wanakosa nafasi ya kuonekana timu taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa sababu kubwa ni kwamba ligi ya muungano hakuna na ni sababu tosha ya kutoonekana kwa wachezaji hao mfano mzuri miaka ya Nyuma kulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa wakicheza timu ya taifa kama akina Haroub ,Hafidh Ally ,Hassan wembe ,Juma Bakari Kidishi ambao hawa walionekana mara baada ya kucheza katika timu ya taifa ya Tanzania na walikuwa wakicheza katika Vilabu vyao vya Unguja na Pemba ambavyo vilikuwa vikishiriki Ligi hiyo.

 Pengine kwa Vijana wa Leo ambao hawajui ngoja nitaje Baadhi ya Timu ambazo zilikuwa zikitishia Hata amani ya katika soka ya Tanzania kutoka Zanzibar ,Malindi,Shangani,KMKM Small Simba ,Mlandege  timu hizi  zilikuwa zikizipa tabu timu za Tanzania Bara kwa soka safi na Hata Bara kulikuwa na timu Nyingi ambazo Leo hii zimebaki kuwa Magofu ,kama Pan Africa,Cigarate,CDA,Ushirika na Nyingi nyinginezo ambazo leo hii kama kuna bahati kunaweza kuwa kumebaki viwanja tu ambavyo vinatumika na timu nyingine tofauti na sio zile za kihistoria .

Kikubwa katika jambo hili tuliweza kuona ushindani wa kweli mpaka timu za Zanzibar kuna wakati ziliweza kushiriki hata hatua ya Robo fainali kombe la washindi kwa kukaa pamoja na watu wa Bara na kukubalina kuwa Zanzibar icheze kombe la Washindi na Tanzania Bara icheze klabu bingwa Maneno haya siyo kwangu ni ya Abdallah Maulid akiwa pamoja na Mwalusako .
Mimi sipingani nao kwani nia ya kuleta mashindano hayo tena kwanza kutarejesha undugu,lakini wachezaji wataweza kusomana na kujuana Tabia zao na Kutembeleana na kubadilishana uzoefu  kwa sasa timu na wachezaji hawa wanataka kufanya Tamasha ambalo litawaleta wazee wazamani wa afrika mashariki pamoja ili waweze kukaa pamoja na kufanikisha mambo mengi ya kisoka na kuwa shawishi watu kuwa na uelewa wa ligi ya Mungano.

Ambayo ilikufa baada ya Zanzibar Kupata nafasi ya Mpito ya timu zake kushiriki michuano ya  klabu bingwa na kombe la washindi Barani afrika na kuifanya michuano hiyo kukosa mashiko kitu ambacho Abdallah maulid na Mwalusako wanasema ni kosa kubwa kuwahi kufanyika katika soka la kisasa 

na wakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wanamashaka na aliyetoa wazo la kufuta ligi hiyo kwani huenda hakucheza soka katika maisha yake .
Timu za Zanzibar zimekuwa hazifanyi vizuri kutokana na kuwa na mipango hafifu na kukosa motisha hasa ya kuidhamini ambapo makampuni yenye fedha kubwa ambayo yaliyo mengi ni Mahsusi kwa utengenezaji wa Pombe hayaruhusiwi Ndani ya Ardhi ya Zanzibar kwani Jamii kubwa ya wakazi wa Zanzibar ni waislamu ambao katika imani yao pombe ni halamu kabisa kwa hiyo siyo vema kutangazaa jambo hilo katika ardhi hiyo Japo Baadhi ya Raia wa Kisiwa hicho hunywa na ni watumiaji wazuri wa Ulabu.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers