HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

1 October 2013

MICHUANO YA CHALENJI KUANZA NOV 27

 
Michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inafanyika Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.

Nchi wanachama ambazo zinataka kushiriki zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu. Wanachama wa CECAFA ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda na Zanzibar.

Michuano hiyo itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na ajenda ya uchaguzi. Uchaguzi huo ni kwa ajili ya kujaza nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Wajumbe wanaomaliza muda wao ni Sahilu Gebremarian wa Ethiopia ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CECAFA, Abdigaani Saed Arab (Somalia), Tariq Atta (Sudan) na Raoul Gisanura (Rwanda).

Majina ya wagombea yanatakiwa kuwa yamewasilishwa katika Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu, na yakiwa yamethibitishwa na vyama vyao vya mpira wa miguu.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers