HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 December 2013

HAMBA KAHLE ' MANDELA AFRIKA HAIJAWAHI KUPATA MTOTO KAMA WEWE

 
Nelson Madiba Rolihlahla Mandela  Rais wa kwanza mweuzi wa afrika kusini ambaye amefariki Dunia usiku wa Desemba 5
Msiba huu ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwa Afrika Kusini, Afrika na Dunia kwa ujumla kutokana na mchango mkubwa wa Mzee Mandela katika mchezo huu.

Mzee Mandela anakumbukwa kwa mchango wake katika Fainali za Afrika (AFCON) zilizofanyika mwaka 1996 nchini Afrika Kusini na hata zile za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini humo mwaka 2010.

TFF tunatoa pole kwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA), Danny Jordan, na wananchi wa Afrika Kusini na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Iconic: Nelson Mandela congratulates South Africa's rugby team captain Franois Pienaar after winning the World Cup in 1995
: Nelson Man'dela akimpongeza nahodha wa timu ya taifa ya afrika kusini  Franois Pienaar baada ya kushinda ubingwa wa Dunia  1995
Ulimwengu wa Michezo umetoa shukrani za kipekee kwa mpiganaji wa kweli wa ubaguzi wa rangi shujaa wa kweli  Nelson Rolihlahla Mandela,ambaye amekufa akiwa na umri wa miaka   95.
Rais wa Africa kusini   Jacob Zuma aliutangazia umma usiku wa jana kuwa Rais wa kwanza mweusi wa afrika kusini Ametangulia mbele ya haki
Ni mmoja kati wa watu mashuhuri zaidi katika michezo katika ardhi ya afrika kusini na duniani kwa ujumla rais huyo wa zamani amekuwa akitoa mchango wake mkubwa katika tasnia ya michezo
Tiger Woods, Mchezaji namba moja kwa ubora wa mchezo wa Golf Duniani anasema kukutana Mandela ilikuwa moja kati ya jambo ambalo sikuwahi kulifanya katika maisha yangu  "".
"Sidhani kama kati yetu asingeweza kushukuru kufanikiwa katika jambo kama hilo .Kuliongoza taifa na kupendwa na Dunia hii inaonyesha yeye ni nani ?  ," Aliongeza .
Na Bingwa wa zamani wa Dunia wa Mchezo wa Ngumi  Muhammad Ali : "Alikuwa mtu aliyetafuta maisha akiwa na sababu Namatumaini ; Tumaini kwake yeye Binafsi ,Nchi yake na Duniani  .
"Aliwavutia watu kwa kuwaonyesha kuwa wanaweza kupata lile walilodhani kuwa aliwezekaniki na sasa linawezekanika."
Taswira ya  Mandela Akibadhi Taji la  Webb Ellis  Springbok rugby  - kama muandaaji na bingwa wa mashindano hayo mwaka  1995 Rugby World Cup - ni jambo linaloonekana kuwa la kihistoria zaidi pale alipoileta Nchi pamoja .

Joost van der Westhuizen,ambaye alicheza fainali ya Mchezo huo amesema ni,siku ya uzuni kwa Nchi yetu alale salama   Madiba. na salamu nyingi za pole kwa familia yake ."

Wanamichezo wetu wa afrika kusini tunatoa salamu za rambirambi kwa mzee Mandela anasema . Golfer Ernie Els : "Ni siku ya Uzuni sana .Ni siku ya Uzuni sana kwa afrika kusini  na Duniani kwa ujumla .Tumepoteza moja kati ya Viongozi bora zaidi katika kipindi hiki .
"Hakuna jambo baya ambalo amelifanya kijana huyu .Alipigania kwa lile aliloliamini  ,Alikwenda jela kwa miaka mingi na alitoka kuja kuliongoza taifa ni baba wa taifa letu na baba wa bara la afrika  
.
". Ni huzuni kubwa sana kwa kuwa alitakiwa kwenda .
"Alikuwa na miaka95 na ameishi maisha marefu na alikuja kutimiza  yale aliyotaka kayala kwa muda mfupi."

SAFRICA-MANDELA-TIGER WOODS
Jambo la kusisimua : Mandela anakutana na  Tiger Woods
Rais wa Mchezo wa Cricket  Africa kusini Chris Nenzani anaongeza : "Katika Demokrasia ya kweli Mandela ametuachia azina ya kizazi na kizazi ambayo watajivunia siku zote .

"Ulimwengu wa michezo utamkumbuka kwa kuunganisha watu kupitia michezo nakuwafanya watu weusi na weupe kucheza kwa moja .".
Usain Bolt : "Ni moja kati ya watu wakubwa ambao siku wahi kuwaona ameondoka  ..Roho yake ilale pahala pema peponi na kwa amani ..ni moja kati ya wapiganaji wakubwa …"

Mwendesha magari wa uingereza  F1  Lewis Hamilton alichapisha pii katika kurasa yake ya kui alipokutana na  Mandela huku akiacha ujumbe: "Moja kati ya vitu vikubwa maishani mwangu ni kukutana na Madiba. ni moja kati ya watu wa kusisimua ambao wamewahi kuishi Duniani & Bila shaka ni moja kati ya watu Bora zaidi ambao nimewahi kukutana nao .Nitamkosa,Tutakukosa Madiba. Mungu akupumzishe salama Upendo wako uishi kama baba alivyompenda mwanae .Pumzika salama .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers