HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 December 2013

DAVID MOYES TUNAWEZA KUTWAA UBINGWA BADO!!


Manchester United leo wamepata kipio chao cha pili mfululizo cha Ligi Uwanjani kwao Old Trafford na hii ni mara ya kwanza tangu Mwaka 2002 wakati Newcastle waliposhinda Bao 1-0 na hii ni mara ni mara ya kwanza kwa Newcastle kushinda Uwanjani hapo tangu Mwaka 1972.
Bao la ushindi la Newcastle lilifungwa na Yohan Cabaye katika Dakika ya 61. 
Man United, ambao leo walibadilisha Wachezaji 7 toka Kikosi kilichofungwa Jumatano, walipata nafasi kadhaa za kufunga pale Patrice Evra alipopiga kichwa na Mpira kupiga posti na nyingine ni majaribio ya Javier Hernandez na Adnan Januzaj yaliyookolewa na baadae Bao la Robin van Persie kukataliwa kwa kuwa Ofsaidi.
Jumatano iliyopita Man United walifungwa Old Trafford na Everton Bao 1-0 na Mechi inayofuata kwao ni hapo Jumanne Desemba 10 watakapocheza UEFA CHAMPIONS LIGI Uwanjani Old Trafford na Shakhtar Donetsk.
Magic moment: Newcastle players celebrate with Cabaye after he bagged what proved to be the winner

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers