HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 December 2013

JE NI MWISHO WA ARSENAL NA MAN CITY ULAYA ?

Arsenal manager Arsene Wenger (left), Chelsea boss Jose Mourinho (second left), Manchester City manager Manuel Pellegrini (second right) and Manchester United boss David Moyes

 Manchester City imepangwa kukutana na  Barcelona katika hatua ya mtoano wa ligi ya  mabingwa Bara la ulaya katika hatua ya kumi na sita Bora .huku mahasimu wao
Arsenal wakipangwa tena na  Bayern Munich.

RATIBA YA LIGI HIYO

  • Michezo ya kwanza itachezwa : 18/19/25/26 February na   11/12/18/19 March (utakuwa Mzunguko wa pili 
  • Robo fainali : 1/2 April na 8/9 April
  • Nusu fainali: 22/23 April and 29/30 April
  • Fainali : 24 May

Chelsea,ambao ni mabingwa wa mwaka   2012 watapambana na  Galatasaray wakati  Manchester United watasafiri hadi Ugiriki kupambana  Olympiakos.


Mechi nyingine za Mzunguko huo , AC Milan watakutana na  Atletico Madrid, Bayer Leverkusen watakwenda ufaransa kumenyana na Paris St-Germain, huku Schalke wakiwa na kibarua kigumu cha kuwazuia mabingwa mara tisa wa ulaya  Real Madrid na  Zenit St Petersburg itakutana na   washindi wa pili wa mwaka jana  Borussia Dortmund.


Chelsea na  Manchester United wao wanafaida ya kucheza mechi za pili Nyumbani baada ya kuongoza makundi yao wakati ,City and Arsenal zitacheza Nyumbani mechi za kwanza na kumaliza Ugenini 

.

  Mtendaji mkuu wa City Ferran Soriano na Mkurugnzi wa ufundi wa Barca  Txiki Begiristain walikuwa wanafanya kazi pamoja na ndiye aliyemuuza  Yaya Toure kwa  City mwaka 2010.

Begiristain ameiambia Sky Sports: "Kuna timu mbili kubwa ,Moja ikiwa na historia kubwa ulaya na nyingine inawachezaji wakubwa wanaochipukia  .

MECHI WALIZOKUTANA BAINA YA  Arsenal na  Bayern Munich

Mikel Arteta
5 Dec 2000 - Arsenal 2 Bayern 2
14 Mar 2001 - Bayern 1 Arsenal 0
22 Feb 2005 - Bayern 3 Arsenal 1
9 Mar 2005 - Arsenal 1 Bayern 0
19 Feb 2013 - Arsenal 1 Bayern 3
13 Marc 2013 - Bayern 0 Arsenal 2

"Ni timu yenye kujiamini baada ya kushinda dhidi ya mabingwa wa sasa katika uwanja wao wa nyumbani na wakiwa na uzoefu wa kutosha kwa kucheza mara mbili nyumbani na Ugenini Dhidi ya Barcelona .

"Barcelona ni mabingwa mara nyingi zaidi lakini tunajiamini ."

Arsenal ilishinda  2-0 ugenini Dhidi Bayern Munich Mwezi  March lakini iliondolewa kwa sheria ya Goli ugenini baada ya kufungwa mechi ya kwanza 3-1 , huku wajerumani wakienda kucheza fainali na ndugu zao Dortmund.


Bayern wamewahi kuiondoa  Gunners mara mbili katika mashindano hayo .

Chelsea itapambana na Mshambuliaji wake wa zamani   Didier Drogba  kwa mara ya kwanza Tangu raia huyo wa Ivory coast kuondoka   Stamford Bridge baada ya kukaa miaka nane  2012.

Kocha Jose Mourinho alikaririwa juma lililopita kuwa mechi hiyo ndiyo aliyokuwa akiitaka .


RATIBA KAMILI :

Manchester City v Barcelona

Olympiakos v Manchester United

AC Milan v Atletico Madrid

Bayer Leverkusen v Paris St-Germain

Galatasaray v Chelsea

Schalke v Real Madrid

Zenit St Petersburg v Dortmund

Arsenal v Bayern Munich

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers