Final Draw reveals intriguing groups

Makundi ya Kombe la Dunia yamepangwa Nchini Brazil siku ya ijumaa huku matarajio ya waafrika wakitamani Baadhi ya timu zao kutokukumbana na Timu ngumu zaidi ambazo zinajulikana kidunia Kwa mtazamo wa Mashabiki wengi wa soka la afrika kuwa ni hatari zaidi .

Kundi A ambalo linatimu za Brazil, Croatia, Mexico, Cameroon  ukilitizama kundi hili sio jepesi wa gumu kwa timu ya afrika unapocheza kombe la dunia lazima ufanye kazi ya ziada kwani katika kumbukmbu zangu hakuna timu iliyotwaa ubingwa wa dunia bila kuifunga timu kigogo hii inaonyesha wazi kuwa afrika tuwaoga sana katika mashindano hasa ya kombe la dunia Wanachotakiwa kukifanya Cameroun ni kujipanga na kutafakari katika kucheza kimahesabu tu na kuwa mechi iliyopo mbele yako na sio ambayo haujacheza siku zote afrika huwa tunahisi kuonewa au kupangwa makundi magumu kitu ambacho sio kweli kwani mara zote timu hupangwa kutokana na Viwango  vya fifa ukiwazatazama wachezaji waafrika wanaocheza ulaya ukutana na wachezaji wanaocheza vilabu hivyo hivyo iweje muwe waoga tunahitaji kujiamni na kufanikisha azma ya kuwa hakuna kisichowezekana ili uchukue ubingwa dunia lazima ufe.
Kundi  C: Colombia, Greece, Côte d’Ivoire, Japan Timu ya ivory coast ambayo imekuwa ikiomba kila  mwaka kuwa isikutane na timu vigogo kwa mtazamo wao wanaweza kufurahi lakini mimi sioni cha kufurahia kwani ukitazama timu walizopangwa nazo ndizo hatari zaidi Colombia inacheza soka kama la Brazil ,Ugiriki hawa ndio waliwahi kumtoa kamasi Cristiano Ronaldo na ureno yake katika fainali za ulaya mwaka 2004 Japana ni timu amabayo inashiriki kombe la dunia kwa takriban mara ya saba ukilinganisha na Ivory coast mara ya pili kwa hiyo inakuatana na timu zenye uzoefu je unafikiri ni kazi rahisi hapana la hasha kazi ni ngumu sana hakuna mchekea kwa timu za afrika zinazotaka urahisi kwani sijui ni nani aliwaambia kombe la dunia ni rahisi wanachaotakiwa kukifanya ndugiu zangu hawa afrika ni kujipanga na kumsikiliza mkufunzi anasema nini na wao ndicho wanachotakiwa kukifuata kiwanjani.  

Kundi F : Argentina, Bosnia-Herzegovina, Iran, Nigeria wawa kilishi wa afrika Nigeria na Mabingwa wa afrika wanakutana tena na Argentina timu walioishinda katika fainali za kombe la Olimpik mwaka 1996 kule Atlanta Marekani wakakutana tena Korea /japan sasa kuna haja gani ya kuiogopa Argentina timu waliyowahi kuifunga fainali najua wanaweza kuzidharau Nchi kama Iran,na Bosnia-Herzegovina na hapo ndipo watakapofungwa kwani wenzao hawadharau timu wanazokutananazo mara nyimngi timu za afrika huwa zinafungwa katika fainali za kombe la dunia kwa kudharau maadui zao kugombania posho kutoka katika vyama vyao  huku wakishindwa kucheza mechi zao wakati fifa inawapa pesa zaidi ya wanazogomea huu ndio ujinga wa afrika.

G: Germany, Portugal, Ghana, USA hata katika kundi hili sioni kama kuna tatizo Ghana ilishacheza na Ujerumani mwaka 2010 nchi afrika kusini katika fainali za kombe la dunia ilishacheza na marekani kwa hiyo inazijua Nje ndani timu inazocheza nazo hakuna haja ya kubabaika ni kujipanga  unapogopa na kuanza kusema kundi gumu hivi hata kama utapewa kundi ujipangie mwenyewe bado utafungwa . kauli yangu ni ile ile tuingie kiwanjani tucheze hakuna jambo jepesi katika dunia hii .

Belgium, Algeria, Russia, Korea Republic nina maliza kwa wawakilishi pekee kutoka katika kanda ya afrika kaskazini nawao wanatakiwa kufanya yale ambayo nimeayaandika kwani kama mpira ni ule ule viwanja ni vile vile huwa nasema siku zote hakuna jambo la hisi swala la msingi ni kushika yale ambayo mwalimu anasema katika vyumba vya kubadilishia na kuachana na dhana ya kusema tunapangiwa makundi magumu kwani hakuna siku tutapangiwa kundi jespesi hata siku moja kwa hiyo rai yangu kuwa timu za afrika kuwa tumeshajua timu tunacheza nazo la msingi ni kutamaza namna zinavyocheza na namna zinavyofundishwa na aina ya mpira wanaocheza tufikirie mechi iliyopo mbele yetu na sio tutakuatana na nani mechi ijayo .  



 Group A: Brazil, Croatia, Mexico, Cameroon
Group C: Colombia, Greece, Côte d’Ivoire, Japan
Group G: Germany, Portugal, Ghana, USA